Pages

Sunday, May 10, 2015

PICHA: Mtoto wa nne wa Mwalimu Nyerere, John Nyerere afariki dunia

John Nyerere (katikati) enzi za uhai wake. MTOTO wa nne wa Mwalimu J.K Nyerere, John Nyerere amefariki dunia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa kapteni wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita. Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia ni kwamba marehemu amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya mapafu na kisukari kwa muda mrefu.
GPL

No comments:

Post a Comment