Pages

Friday, May 22, 2015

Wanawake wa Chechnya wazuiwa Kutumia WhatsApp


Kiongozi wa Chechnya, Ramzan Kadyrov

Nimekutana na hii habari nikafurahi. Wanawake hao wamenyimwa kutumia whatsapp kutokana na binti wa miaka 17 aliyelazimishwa kuolewa..nilipost hii habari huko nyuma tatizo sijajua kuweka link ningeweka hapa..


Kiongozi wa Chechnya Ramzan Kadyrov amewataka wanaume kuwazuia wake zao kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp baada ya mada ya ndoa ya lazima kusambaa katika ujumbe mfupi wa simu.
Kadyrov amekaririwa akisema "wafungieni ndani, msiwaache wakatoka nje, kwa hiyo hawatatuma chochote,"

Bwana Kadyrov mapema aliunga mkono ndoa ya afisa wa Polisi kumwoa msichana wa miaka 17, japokuwa alikuwa tayari
ameolewa, katika tukio la ukiukaji wa sheria za Urusi.

Mnadhimu wake wa kijeshi tangu wakati huo alipendekeza kuhalalisha ndoa ya zaidi ya mke mmoja nchini Chechnya.

Bwana Kadyrov, kiongozi wa kimila na mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika miaka ya karibuni alipiga marufuku kuwachukua kwa nguvu wanawake kwa ajili ya kufunga nao ndoa za umri mdogo.

Pia anafikiriwa kuwa anapendelea ndoa za wake wengi. Msaidizi wake mkuu Magomed Daudov anasema: "hiyo yote inaendana na Sharia. Lakini kama mwanaume anaweza kuhudumia zaidi ya mke mmoja, kwa nini asioe wengi?" Watu wengi katika jamhuri ya ya Urusi ya Chechnya, ni Waislamu.

BBC

No comments:

Post a Comment