Pages

Wednesday, June 3, 2015

Jengo la ghorofa 16 kubomolewa Dar kwa ajili limejengwa chini ya kiwango

JENGO la ghorofa 16 lililopo mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es Salaam linatarajiwa kubomolewa kwa kuwa linadaiwa kujengwa chini ya kiwango.

Amri hiyo imetolewa na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

Uwepo wa jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango limezua hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo,kwani lipo karibu na jengo jingine lililokuwa na ghorofa 16 ambalo lilianguka wakati ujenzi wa ghorofa hilo ukiendelea.

Hatua za ubomoaji jengo hilo zinaendelea wakati wakazi wa eneo hilo  wameombwa kuepukana na madhara yatakayojitokeza katika ubomoaji huo.

Kampuni ambayo imepewa dhamana ya ubomoaji wa jengo hilo ni  kampuni ya  Kichina ya ERJE ambayo tunasubiri itekeleze wajibu wake katika kubomoa jengo hilo.

MICHUZI

No comments:

Post a Comment