Pages

Wednesday, June 3, 2015

Kuoa hakutaathiri mziki wangu - Luteni Kalama

Luteni Kalama, star wa muziki ambaye wiki iliyopita alimvisha pete ya uchumba rasmi mpenzi wake wa siku nyingi, mrembo aliyewahi kushikilia taji la Miss Ruvuma Bella amewahakikishia mashabiki wake kuwa hatua ya kufunga ndoa anayonuia kuichukua hivi karibuni, haitaathiri kabisa muziki wake.

Kukiwa na mifano dhahiri ya wasanii kadhaa walioshuka ama kuweka sanaa pembeni baada ya jukumu la ndoa na familia kuingilia kati, Luteni amesema kuwa kama kipaji cha mtu kipo hakiwezi kupotea, akijiamini kuwa jina la Luteni Kalama litabaki siku zote katika sanaa.

Vile vile staa huyo akazungumzia ujio mpya wa kundi la Gangwe Mob, akiweka wazi kuwepo kwa rekodi kama 3 ambazo zitatoka kati ya sasa na mwezi wa 7

EATV

No comments:

Post a Comment