Pages

Saturday, June 20, 2015

MAJAMBAZI 7 YAMUUA MFANYABIASHARA NA KUMPORA SH LAKI 3!!

MAJAMBAZI 7 wakiwa na silaha mbalimbali wamemuua kwa kumpiga risasi mfanyabiashara Felix Laungeni (58) ambaye ni mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jafari Ibrahim alisema kuwa watu hao walitoweka mara baada ya tukio hilo. Kamanda Jafari alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 18 mwaka huu majira ya saa 1:30 usiku huko Tanita kata ya Mkuza tarafa na wilaya ya Kibaha.

Imeelezwa kuwa watu hao wakitumia bunduki aina ya shotgun walimpiga risasi tumboni na kwenye kidole na kumpora fedha taslimu kiasi cha Sh 300,000 za mauzo ya siku hiyo na simu aina ya Tecno.

Alisema mbali ya kuwa na silaha hiyo pia walikuwa na silaha zingine yakiwemo mapanga kisha kutoweka pasipojulikana. Alisema kuwa marehemu alikufa Juni 19 mwaka huu alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Aliwataka watu waliokuwa na taarifa juu ya watu kuta taarifa ili watiwe mbaroni.

HABARI LEO

No comments:

Post a Comment