Pages

Tuesday, June 2, 2015

Mbunge wa Ukonga, Eugene Mwaiposa Afariki Dunia


MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwamba marehemu alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.

Ameongeza kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Shughuli ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.

GPL

No comments:

Post a Comment