Pages

Friday, June 12, 2015

MKAZI WA MBEZI AFIKISHWA KORTNI KWA KUMLAWITI MTOTO WA MWAKA MMOJA

MKAZI wa Mbezi Beach Dar es Salaam, Tuntutye Mwasyete (25), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumlawiti mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mbele ya Hakimu, Lilian Rutehangwa, Wakili wa Serikali Masini Musa alidai kwamba tukio hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu huko Kawe.
Mtuhumiwa alikana shtaka hilo na alirejeshwa mahabusu hadi Juni 24 mwaka huu yatakaposomwa maelezo ya awali.


MTANZANIA

No comments:

Post a Comment