Pages

Monday, June 1, 2015

MWAKYEMBE: Lowassa hana sifa ya kuwa raisi

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, ameapa kupambana kufa au kupona, kumzuia Edward Lowassa, kuingia Ikulu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Katika andishi lake alilolituma kwenye mitandao ya kijamii, Dk. Mwakyembe anasema, Lowassa hana sifa ya kuwa Rais wa Jamhuri. Amesema,
“…namuona Lowassa kama mtu ambaye anatapatapa huku akiujua ukweli kwamba hana nafasi hata kiduchu ndani ya CCM.”

Nalisema hili bila kukemea jicho wala kuwa na wasiwasi wowote na maisha yangu kwani najiamini na Mwenyezi Mungu ananilinda na watanzania wananiombea daima na najisikia furaha kuwa miongoni mwa wabunge wa CCM ambao hatukuufumbia macho ufisadi wa kampuni feki la kuzalisha umeme iliyomuhusisha waziri mkuu ambaye mimi namuita aliyejiuzulu na sio kustaafu.

Nakushauri ujitafakari vizuri kwani CCM haitoweza kumkabidhi nduli nchi hii.
Unahaha kutumia mabilioni kuhonga na kusafirisha watu kwenye tendo la kutangaza nia tu, hivi unafijiri kamati zote za CCM zina njaa ya pesa zako za kifisadi?

Hivi hujui watanzania wanakushangaa unasema safari ya matumaini wakati safari hiyo ni ndani ya bahari iliyojaa majoka na mizimu ambayo imejivika ngozi ya kondoo ili iwameze katikati ya bahari?

Nitakuwa wa kwanza kujitafakari na kuitafakari CCM na kuchukua hatua ambayo najua watanzania wasiouza utu wao kwa dhamana ya fedha.

Ninakusubiri kwa hamu ili nikusikie utakavyokuwa unabadili jihanam kuwa peponi, kwa manufaa ya watanzania nitaanika hadharani uozo wako wote kwa ujasiri na bila hata chembe ya woga ili watanzania wasipotoshwe tena kwa njia ya nbwembwe za fedha. Eh mwenyezi mungu nipe uthabiti kwa hilo.

Rai yangu kwa wana CCM na watanzania tuchague viongozi bora na sio kwa nguvu ya fedha, wapambe na kutembelea nyota ya mtu.

Utauficha wapi uso wako wakati ambapo CCM itakapokuangusha kwa kishindo na kuchagua wawakilishi walio safi? Utapata kiharusi na shock bure kwa kupoteza fedha za madili uliyopiga RICHMOND na ufisadi mwingine.

Hon Dr. Harison Mwakyembe (Mb) Waziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
CHANZO MWANAHALISI

No comments:

Post a Comment