Pages

Thursday, June 11, 2015

Nikikatwa nitampigia kampeni Mwandosya - MEMBE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kama CCM haitampitisha kuingia tano bora, atampigia kampeni kwa moyo wa dhati Profesa Mark Mwandosya iwapo ataingia fainali ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.

Membe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama   wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya waliojitokeza kumdhamini.

Alisema unapozungumzia viongozi waadilifu nchini, Profesa Mwandosya ni namba moja, kwani amekuwa kiongozi mwenye maadili ya uongozi na mwenye upendo wa dhati kwa wengine.

“Natamka hili kwa moyo wangu wa dhati, jina langu lisiporudi ndani ya chama, nitampigia kampeni Profesa Mwandosya. Sina tatizo lolote hata  wakisema  mimi nimuachie  Mwandosya nipo tayari, kwani ndiyo viongozi  wanaotakiwa kama yeye  kwa sasa kuongoza nchi yetu,” alisema.

Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mmoja wa wagombea urais kwa tiketi ya CCM. Wagombea wengi wamekuwa wakieleza kuwa wameamua kuingia kwenye mbio hizo kwa kuwa hawajaona mgombea mwenye sifa zaidi yao.

MWANANCHI

No comments:

Post a Comment