Pages

Tuesday, September 15, 2015

Tabia 8 za watu ambao nyumba zao ni safi kila wakati

Hebu jiulize kidogo  kama mgeni akikutembelea bila taarifa unajisikia aibu kwa jinsi nyumba ilivyo. Kama ndiyo basi inaonekana una nyumba isiyokuwa safi kila wakati.
Fikiria ni kwa jinsi gani zaidi ungeweza kuwa na maisha ya raha kama ya watu wenye nyumba ambazo inachukua dakika 15 tu kuweka kila kitu sawa na hivyo nyumba yote kuonekana nadhifu.
Nimetafiti tabia za kila siku za watu  wenye nyumba safi
– zingatia neno “tabia.” Nilichogundua  ni kwamba inahitajika usafi na mpango wa kila siku kuifanya nyumba iwe nadhifu.
Soma hapa ugundue tabia hizi nane ambazo watu wenye nyumba nadhifu wanazo, na huenda ukaamua kuziasili ili kukuwezesha kutoka kwenye nyumba isiyo nadhifu ambayo umekuwa ukiishi:
         1.    Tandika Kitanda
Kabla hujaondoka chumbani au nyumbani asubuhi hakikisha unatandika kitanda chako.

2.     Usiache vyombo vichafu jikoni
Kila wakati ambao jiko halitumiki kusiwe na vyombo vichafu. Kufanya hivi kuweka jiko safi na pia kunarahisisha maandalizi ya kupika chakula kingine.
3.     Weka utaratibu wa kufua nguo
Kuwa na utaratibu wa kufua nguo chafu kunasaidia zisijilimbikize. Nguo chafu zinapokuwa nyingi ndani ya nyumba kuleta muonekano wa mrundikano hasa kwa wale wenye familia kubwa.
4.     Tumia vikapu au vitenga kuweka mpangilio
Kunapokuwa na sehemu kwa kila kitu, ni rahisi kuweka kila kitu mahali pake. Tumia vitenga na mashelfu kwenye kila chumba kwa ajili ya kuhifanyia vitu vikubwa na vidogo.
5.     Fungua vitu vipya kutoka kwenye maboksi yake
Kitu kipya kinapoletwa nyumbani kikiwa ndani ya boksi, kifungue ukiondoe kwenye boksi na ulitupe mara moja.
6.     Usitupe nguo sakafuni
Hili ni jaribu kwa wengi baada ya mihangaiko ya siku nzima jinsi gani wanahifadhi nguo walizokuwa wamevaa. Kuendana na maisha ya siku nzima ya mhusika, nguo walizovaa siku hiyo watu wenye nyumba nadhifu wana tabia ya kuzikunja, ama kuzitundika ama kuziweka kwenye kapu la nguo za kufua badala ya kuzivua na kutupa sakafuni. Kufanya hivi kutawezesha sakafu na nguo kwa pamoja vionekana safi.

7.     Safisha kadri unavyotumia
Unaweza kupunguza kiasi kikubwa cha uchafu kama utasafisha kadri unavyotumia. Kama utasuuza ubao wa kukatia baada ya kuutumia wakati nyama ikichemka au kuosha vyombo wakati wali ukiiva, vyombo vingi vitakuwa safi utakapofika wakati wa kupakua chakula.
8.     Kamwe usiende kulala ukiacha jiko chafu
Kataa tabia ya kukimbilia moja kwa moja kitandani  baada ya mlo wa usiku.  Hakikisha unasafisha jiko lote usiku – osha vyombo, futa kaunta na fagia sakafu mabaki yoyote ya chakula yaliyodondoka. Hi pia itasaidia kutokaribisha panya na mende jikoni.
Kwa maoni au maswali tembelea www.vivimachange.blogspot.com


No comments:

Post a Comment