Pages

Friday, October 16, 2015

Mitindo mitano ya masinki ya kisasa ya jikoni

Mtindo au muundo wa sinki la jikoni ni muhimu uendane na ukubwa na matumizi ya jiko. Ifuatayo ni miundo mitano ya masinki ya jikoni na matumizi yake
Hili sinki ni kubwa lakini lina karai moja na sehemu ya kuwekea trey la kukaushia vyombo. 
Sinki hili ni dogo kuliko yote na lina sehemu ya karai peke yake. Hili linafaa zaidi  kwa jiko la mtu mmoja au wawili tu
Hili sinki ni dogo lakini lina karai moja na sehemu ya kuwekea trey la kukaushia vyombo. 


Sinki hili lina makarai mawili moja kubwa na kingine kidogo pia kuna sehemu ya trei. Hili ni kwa jiko la saizi ya kati kwa matumizi ya watu watano
Sinki hili lina makarai mawili makubwa yenye ukubwa unaolingana. Mtindo huu ni sahihi kwa jiko kubwa na ingekuwa mimi kati ya mitindo yote mitano ningechagua huu

No comments:

Post a Comment