Pages

Monday, November 16, 2015

JINSI YA KUTANDIKA MAZULIA YA NYUMBANI

Mazulia ya nyumbani naweza kuyaweka kwenye makundi manne kutokana na ukubwa wake. Yapo yale ya wall to wall, yapo makubwa ambayo sio ya wall to wall, yapo madogo ya kutupia kwa mfano kwenye corridor ama pembeni kwa kitanda na yapo madogo ya kukanyagia mlangoni, bafuni na kadhalika. Kwenye utandikaji wa leo nitazungumzia kundi la yale makubwa lakini sio ya wall to wall.
Unapotandika carpet hakikisha fenicha zinakaa juu yake. Njia ya kwanza hapo juu ndio sahihi, Ya pili ni hapana.

Zingatia ukubwa wa carpet na ukapotaka kulitandika carpet lako kwa mfano kama ni dining hakikisha meza na viti vitatoshea juu ya carpet husika. Kwahiyo kuwa makini usijenunua ambalo ni dogo sana.

 Pia kama chumba tayari kina carpet la wall to wall basi lile la juu yake lisiwe
kubwa kiasi cha kufunika hilo cha chini.
Chagua carpet la rangi partten na maua kuendana na mapambo mengine ya unapotaka kuliweka.

NYONGEZA YA MAKALA

Makosa matano ya kuepuka kuhusiana na mazulia ya nyumbani
Mazulia ya nyumbani naweza kuyaweka kwenye makundi manne kutokana na ukubwa wake. Yapo yale ya kufunika ukuta kwa ukuta, yapo makubwa lakini sio ya kufunika ukuta kwa ukuta, yapo madogo ya kutupia kwa mfano kwenye ujia ama pembeni kwa kitanda na yapo madogo kabisa  ya kukanyagia mlangoni, bafuni na kadhalika. 

Kutokana na makundi haya manne yakupasa kuepuka makosa yafuatayo:
1. Epuka kuchagua zulia ambalo ni dogo sana.
Maana yake ni kwamba utakapotandika zulia dogo na chumba kitaonekana kidogo. Inatakiwa zulia lako liweke mipaka, na msingi wa fenicha zilizo juu yake. Hapo sebuleni zulia linatambulisha eneo la maongezi kwa hivyo linatakiwa kuwa na ukubwa wa kutosha kiasi kwamba miguu ya mbele ya sofa zako inatakiwa kuwa juu ya sofa na moja kwa moja miguu ya aliyekalia sofa itakuwa inakanyaga zulia. 
Vilevile chumbani unataka kupata hisia za zulia kwenye miguu yako. Kama sio zulia la ukuta kwa ukuta huna haja ya kuweka ambalo linaishia mvunguni, badala yake weka madogo kwenye pande mbili za kitanda.

2. Epuka kununua zulia lisilo na muundo wa chumba unachotaka kulitandika.
Maana yake ni kwamba chumba ambacho kina upanda wa mduara, zulia la muundo wa mduara au yai litafaa zaidi na vilevile chumba cha pembe nne zulia la pembenne ni sahihi zaidi. Endapo chumba ni kirefu na chembaba na hujapata zulia maalum la hivyo basi nunua linalouzwa kwa kukatiwa kwa mita na ndipo mtaalamu anaweza kukuwekea upindo kwenye eneo lililokatwa.

3. Epuka kuacha zulia la kufunika ukuta kwa ukuta bila vitupio.
Endapo umeweka zulia la kufunika ukuta kwa ukuta la rangi moja, badi usiliache hivyohivyo. Tupia zulia ndogondogo maeneo ili kukivuta chumba kati na kutengeneza mipaka ya fenicha zilizo mahali hapo ili kuleta mvuto.

4. Epuka kuoanisha rangi ya zulia na kila kitu
Maana yake ni kwamba, kwamfano una zulia la kijivu, sofa za kijivu na pazia za kijivu ni kuwa chumba kitapooza. Ndani ya chumba rangi tofauti ila zenye ujirani zinakuwa na mvuto zaidi.

5. Epuka vizulia vya mlangoni na bafuni visivyokuwa na mpira chini.
Iwapo kizulia cha mlangoni hakina mpira ule wa chini wa kushikana na sakafu, na kinawekwa mahali kwenye salafu ya marumaru au mbao kuna uwezekano mkubwa wa kuteleza na kumuangusha mtu. Hali kadhalika na bafuni.

Kwahivyo msomaji wangu kumbuka kuwa zulia linaunganisha chumba, jitahidi kuepuka mambo haya matano ili upate matokeo unayotaka.

Makala hii imeandaliwa na Vivi. Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani na unataka Watanzania waijue? Tuwasiliane kwa simu/whatsapp 0755200023


No comments:

Post a Comment