Pages

Thursday, November 19, 2015

-----VITU VIZURI------BAFU LA JACUZZI

Jacuzzi ni bafu kubwa lenye muundo wa mabomba kwa chini yake kwa ajili ya kuupa mwili masaji (Massage).Ni zaidi ya bafu la starehe kuwa nalo nyumbani kwa kuwa lina faida nyingi kiafya. Wataalam wa afya wanasema kuwa kukaa ndani ya bafu la Jacuzzi kuna faida za kimwili na kiakili.
Maji ya moto na presha kwenye Jacuzzi yanasaidia kuboresha msukumo wa damu na hewa mwilini hasa kwa wazee na hatimaye wanapata usingizi mnono wa usiku.
 Jacuzzi linaweza kuwa njia sahihi ya kuponyesha misuli na viungo (joints) vinavyouma. Maji kwenye mabomba ya Jacuzzi yanaruhusu presha kubwa ambapo unaweza kuyaelekeza kwenye eneo unalotaka kufanyia massage aidha kwa kusogea ili kupata ule msukumo mkubwa kabisa wa maji. Jacuzzi pia linasaidia kuondoa maumivu ya mwili yatokanayo na michezo.
Kwa wale wanaoteseka na ugonjwa wa rheumatism wanapata ahueni kwenye presha ya maji ya Jacuzzi baada ya kukaa ndani yake kwa dakika chache.

Kutumia bafu la Jacuzzi kunakuondolea msongo wa mawazo. Kama unataka kuburudisha mwili kwa muda tumia bafu la jacuzzi.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023

No comments:

Post a Comment