Pages

Friday, January 29, 2016

HOME DECOR HAPA NA PALE:...DARI LA RANGI, SHELFU ZA VYOMBO, GROUT

Friends, ni post nyingine tena ya kuangalia kunani hapa na pale kwenye mapambo ya nyumba, enjoy!
Hizi ni dari za rangi, kuna wenye nyumba wanaopenda rangi kiasi kwamba wanaweka hadi kwenye dari. Kwa picha hizi unaweza pata idea ya namna dari za rangi zinavyokuwa. Niliweka post hapa hadi wapo wanaoweka wallpaper darini. Kumbuka ni nyumba yako ladha yako.
Wakati mwingine kama kuna uhakika wa usalama hasa familia zenye watu adults shelfu za wazi za kuhifadhia vyombo zinafaa kuliko makabati. Kwanini? Kwasababu kwanza, uzuri wa mpangilio unaonekana halafu pia ni rahisi kutoa na kuweka vyombo. Nitakapofikia umri fulani nadhani nitaenda na open shelf jikoni..ha hahaaaa. Tuombe uzima

Grout ikichafuka au kumeguka unaweza kujikuta unachukia floor yako. Ila habari njema ni kwamba kwa tiles hizo hizo unaweza kufanya marekebisho kwa kuweka grout mpya. Grout mpya ni wazo zuri zaidi hasa bafuni kwenye zile tile za chini ambapo grout inabadilika rangi au kuchakaa kwa ajili ya maji na uchafu. Usilichukia bafu, unachotakiwa ni kujaza grout upya.

Niambie hapa na pale kwenye mapambo yako ya ndani kunani?..Tuwasiliane

No comments:

Post a Comment