Pages

Saturday, January 9, 2016

HOME DECOR HAPA NA PALE:...UJUMBE WA WEEKEND, KITANDA CHA MTOTO, RANGI NZURI ZA NDANI, MATAIRI

Ujumbe mzuri sana hasa kwa jinsia ya KE. Nyumbani kwako ndio mahali penye faragha yako zaidi kuliko maeneo mengine yote na ndipo pa kujidaia. Furahia weekend ukiwa katika muonekano wowote ule.
Kitanda hiki chenye muundo wa gari (Car Bed) kutoka Pexiel Furnitures mtoto yeyote hasa wa kiume lazima atakifurahia. Kama alikuwa anasumbua kulala hapa unakuwa umempata kiulainii.
Nimependa color combination ya nyeupe na jamii ya chocolate inavyoweza kupendeza pamoja. Kama ulikuwa unatafuta rangi nzuri za ndani unaweza kufikiria muunganiko huu. 
Photo credit: ig ya designer_lb
Matairi chakavu yanazidi kuwa kivutio cha bustani kwa kuwa styled kwa njia mbalimbali, nawe nenda na wakati kwa kupendezesha bustani yako na matairi. Haijalishi ukubwa wa bustani.


No comments:

Post a Comment