Pages

Tuesday, January 26, 2016

MBWA ANAWEZA KUWA NI WA PAMBO, HOBBY, BIASHARA AU ULINZI.....Amini usiamini anauzwa hadi dola 800!

Neema akiwa na mbwa wake scooby kwenye gari. Anasema scooby ni mpole anasafiri naye hahangaiki, mkewe ni mjamzito kwahivyo anategemea kupata wajukuu soon..lol

Binafsi kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara ni kwamba sipendi mbwa, lakini navutiwa kusikiliza stori za wanaomiliki mbwa ili kujua kwanini wanafanya hivyo. Hapa kuna hii stori toka gazeti la mwananchi inayosema..VENANCE MWAMOTO: Baada ya kukosa ubunge nilifuga na kuuza mbwa

Tumezoea kuona mbwa akifugwa katika nyumba nyingi kwa lengo la kusaidia ulinzi katika nyumba hiyo. Agharabu wengine hupendelea kufuga mnyama huyo kama rafiki pia kama pambo. Hali ni tofauti kwa mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto ambaye ameamua kufuga mnyama huyo kwa ajili ya biashara na huwatunza kisha kuwauza kwa lengo la kujiongezea kipato. 

Mwamoto ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005 anasema, alianza ufugaji baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.“Katika maisha yangu siku zote nimezoea kufanya shughuli mbalimbali kwa lengo la kujiongezea kipato na siyo kubweteka na kusubiri kazi moja, ndiyo maana najishughulisha na kilimo na ufugaji.Mwamoto anasema, alianza kufuga mbwa wawili wa jinsi tofauti na baada ya muda waliongezeka na kuwauza.

Anasema anawauza mbwa hao, Rwanda na Burundi pamoja na kwenye kampuni za migodi. Mbwa mkubwa huuza kwa Dola za Marekani 800 sawa na Sh1,400,000 za wakati kwa wadogo huwauza kwa Dola 200 (Sh450,00).Mwamoto anasema mbwa anaowafuga ni maalumu kwa ajili ya ulinzi na inamlazimu kuwapa mafunzo maalumu tangu wakiwa wadogo.

Hata hivyo, hakuna kazi isiyokuwa na vikwazo, Mwamoto anasema changamoto kubwa anayokumbana nayo ni kebehi, kusema vibaya na kuchekwa, huku wengine wakimhusisha na kula nyama ya mbwa.“Mimi ni Mhehe watu wengi wanaamini sisi tunakula mbwa, hivyo napata wakati mgumu kwani watu wananikebehi na kunikashifu kuwa nafunga mbwa kwa ajili ya chakula, lakini hilo halinivunji moyo na naichukua hiyo kama changamoto ya kuongea juhudi zaidi.”

Kama na wewe unamiliki mbwa hebu nishirikishe je ni wa pambo, hobby mlinzi au  biashara? Tuwasiliane 0755 200023

No comments:

Post a Comment