Pages

Thursday, February 25, 2016

VIVI MACHANGE HOMES: Project ya kuboresha bustani

Project yangu ya sasa ni maboresho ya hii bustani. Nasubiri kwa hamu kuona matokeo mwenye nyumba anayotaka. Rafiki, je una popote panapokutatiza kuhusu muonekano wa nyumbani kwako? Nitakushauri utapata uelewa na nitakuunganisha na watu wa kukufanyia kazi yako na mwishoni utapata matokeo unayotaka tena kwa gharama nafuu mno. Karibu
Kilicho kizuri tunakiendeleza na palipopwaya tunapafanya pawe pazuri. Kwa mfano haya magimbi yanapendeza sana lakini angalia zile canadian grass kule chini zinakufa kwakuwa zimezidiwa kivuli.

Palm linapendeza ila tutaliongezea maua ya rangirangi kupunguza kijani.
Garden entrance inavutia ila tutaiongezea maua iwe na muonekano wa kibustani zaidi.

No comments:

Post a Comment