Pages

Monday, March 7, 2016

Faida 4 za wallpaper ambazo huwezi ukazidharau

Ubunifu ni sanaa, na namna ambavyo unapendezesha mahali unapoishi ndio mfano hai wa jambo hili. Wakati unapoamua kupendezesha ukuta wa nyumba yako unaweza kuchagua kati ya rangi na karatasi za ukutani zijulikanazo zaidi kama wallpaper. Vitu vingi kama rangi, mguso, michoro na maua unaviangalia wakati huo. Ila ukiamua kuweka wallpaper unapata vitu hivi vyote kwenye kifurushi kimoja.

Kubandika wallpaper ndio hata rahisi zaidi ukilinganisha na mchakato mzima wa kupaka rangi.
Hapa naorodhesha faidia 4 utakazopata kutokana  na kubandika wallpaper kwenye ukuta fulani wa nyumba yako. Faida hizi ni za msingi na si za kudharau:

·         Zinadumu muda mrefu - Zinafaa kwa matumizi yoyote na kwa mtu yeyote katika chumba chochote iwe ni bafuni, chumba cha kulala au cha chakula. Wallpaper inaweza kudumu hadi miaka 15 na hata ukuta ukipata alama ndogo za nyufa, kwenye wallpaper hazitokezi.

·         Rahisi kusafishika - Ni rahisi mno kusafisha wallpaper kwa kitambaa kilicholoa. Hii inakusadia kuondoa vumbi au uchafu mwingine kwa haraka mno bila kuacha alama yoyote ukutani. Na nzuri zaidi unaweza kuchagua aina ya wallpaper ambayo ni ngumu kiasi kwamba unaweza hata kusafisha kwa sabuni na brashi.

·         Ni rahisi kubandika na kubandua - Huenda nawe ni mmoja wa wanaohofia kuwa kubandika au kubandua hizi karatasi za ukutani kutasababusha uharibifu wa ukuta. Sii kweli, nyingi ni rahisi tu kubandua na kubandika tena kama umeamua kubadili muonekano kwa kubandua za zamani na kubandika mpya.

·         Gharama nafuu - Endapo utaamua kubandika wallpaper ni kwamba baada ya muda utagundua kwamba ingekuwa ni kupaka rangi ungetumia gharama kubwa zaidi. Hii ni kwasababu wallpaper zinadumu miaka mingi ukutani kinyume na rangi. Pia kama unataka dunia zote mbili yaani ya wallpaper na ya rangi basi kuta fulani za chumba unabandika karatasi wakati zile nyingine unapaka rangi.

Uamuzi wa kuingia kwenye ulimwengu wa wallpaper ni wako wewe mwenye nyumba!


Ninakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Piga/whatsapp 0755 200023

No comments:

Post a Comment