Pages

Monday, March 14, 2016

Jinsi ya kuchagua muundo wa ngazi za nyumba

Ngazi ni eneo muhimu la nyumba ambalo linawasaidia wakaaji wa nyumba hiyo kwenda maeneo mengine ndani ya nyumba husika, hasa pale nyumba inapokuwa ni ya ghorofa. Mbali na hilo, muundo wa ngazi pia unahusika kwenye kupendezesha nyumba.

Mhandisi David Sembuyagi anasema kuna aina nyingi za ngazi. Ngazi ni gharama na pia ni ngumu kuzijenga. Kwahivyo ni muhimu ukafahamu hayo wakati unapochagua muundo wa ngazi. Kama upo kwenye mchakato wa kujenga nyumba itakayohusisha ngazi basi makala haya yatakusaidia kuamua muundo wa ngazi ambao utakufaa. Dondoo hizi zitakufanya uje na uamuzi wenye uzito:

1.      Bajeti
Miundo mbalimbali ya ngazi ina gharama tofauti. Bajeti yako itaamua mtindo, muundo na malighafi ya kutengenezea ngazi zako.

2.      Nafasi
Nafasi iliyopo ndani ya nyumba inayohusika kwa ajili ya kuweka ngazi inatakiwa kuangaliwa kwani ndio inaamua muundo wa ngazi utakaofaa. Kama nyumba ni ndogo, ni vyema kuchagua muundo wa ngazi ambao hautachukua nafasi kubwa. Na kwa upande mwingine kama nafasi ni kubwa basi unaweza kuchagua ngazi ya muundo wa kuvutia na kubwa, au pia unaweza unaweka mbili upande huu na ule.

3.      Usalama
Kwenye usalama wa ngazi ni lazima kuzingatia mlalo na mwinuko wa hatua usiwe mkali, na pia kizuizi cha pembeni ni muhimu hasa ngazi inapokuwa ni ndefu na ni lazima kwa ngazi ya kupanda ghorofani.  Usalama wa ngazi pia uzingatie uwepo wa watoto na wazee ndani ya nyumba. Upana uwe wa kutosha kuweza kupishana watu wawili,  anayeshuka na anayepanda.

4.      Malighafi
Malighafi kwa ajili ya kutengenezea ngazi zipo za aina kadhaa. Mwenye nyumba anaweza kuchagua ngazi ya malighafi ya chuma, mbao au tofali kwa ajili ya nyumba za kisasa. Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa malighafi zinazochaguliwa zitaendana na muonekano mzima wa nyumba, ubora uzingatiwe kwani malidhafi dhaifu hazifai kwa kutengenezea ngazi.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023

No comments:

Post a Comment