Pages

Wednesday, April 6, 2016

Rangi za nakshi kwa ajili ya ukuta wa nje wa nyumba kutoka Aqua Deco

Kuna cha ziada katika kuchagua muonekano wa ukuta wa nje wa nyumba badala ya kuamua tu kupaka rangi nyeupe kwa mfano. Kwa nyakati za sasa wenye kujenga wengi wanapendelea kuweka  kuta za nje za nyumba zao katika hali ya ukisasa zaidi. Mbali na rangi laini za kawaida  zilizozoeleka toka zamani ambazo ni maarufu kwa kuta za ndani, kuna rangi mpya nyingi za nakshi kwa ajili ya
ukuta wa nje wa nyumba.

Ahmed Salim  ambaye ni mtaalam wa nakshi hizi kutoka Aqua Deco Kijitonyama 0712 792 909 anatujuza kama ifuatavyo, twende tuelimike pamoja msomaji wangu.
Tunaangalia aina 4 za rangi za nakshi kwa ajili ya ukuta wa nje wa nyumba. Nyingi ya nakshi hizi ziko rafu jamii ya mawemawe ambazo kwa majina ni drewa, silkoretasit, crystone na wallmaster. Nakshi hizi nne zimetengenezwa maalum kwa  ajili ya ukuta wa nje kwa sababu zina uwezo wa kustahimili hali ya hewa yoyote na zinadumu kwa zaidi ya miaka 15. Kati ya hizi aina 4 zinazopendwa zaidi Tanzania kwa sasa  ni drewa, wallmaster na crystone.

Drewa ni nakshi za mawe makubwa ya asili yaliyosagwa na kuzalisha mawe madogodogo mithili ya ukubwa unaozidi kidogo punje za mchanga wa mtoni.  Nimetofautisha kabisa kwa kusema mchanga wa mtoni kwani michanga mingine kwa mfano wa baharini una punje ndogondogo sana. Vimawe hivyo vinakuwa vimegandishwa pamoja na kutoa muonekano wa rangi kwenye picha kubwa. Watanzania wengi wanaojenga nyumba za kisasa wanaonekana kupendelea drewa kwenye kuta za nje.

Nakshi ya silkoterasit ikipakwa/bandikwa ukutani inafanya muonekano mlaini na rafu. Yale maeneo laini yana mng’ao.

Crystone ni malighafi za punje zilizotokana na mawe yaliyosagwa, kwakweli inapendeza, itakuondoa katika hali ya kupaka rangi jengo lako mwaka hadi mwaka. Tofauti na drewa ni kwamba japo ukuta unakuwa na nundunundu lakini mguso wa juu ni mlaini. Crystone Ina kemikali za kuzuia fangasi na inadumu hadi miaka 25. Bila shaka msomaji wangu utakuwa umeona nyumba zilizopakwa nakishi hii ya crystone.

Wallmaster ni nakshi ambayo malighafi yake ya awali inakuja kwa mfumo wa unga. Kimuonekano inakaribiana na silkoterasit.

Kwa hivyo kwa hizi nakshi 4 ziko kwenye jamii ya rangi nyingi mno zaidi ya 100, yaani kwa mfano nakshi ya drewa unaikuta kwenye rangi mbalimbali vivyohivyo na nakshi zingine 3 zilizobakia. Kwa maana hiyo kabla hujachagua rangi ya nakshi chukua muda kutafakari muonekano unaotaka. Kuna mwenye nyumba ambaye anapendelea kupaka ukuta wote nakshi ya rangi moja, na kuna ambaye anapendelea kupaka sehemu kubwa ya ukuta rangi moja halafu kwenye kona, msingi na kuzunguka madirisha akapaka nakshi ileile lakini kwa rangi nyingine. Hii  ni ili tu kufanya nyumba ivutie kwa ladha yake mwenye nyumba anavyotaka. Mara nyingi inategemea pia na jinsi usanifu wa nje ya nyumba ulivyo. Kuna nyumba kwenye ujenzi kona zinakuwa tayari zimeshanyanyuliwa kuliko maeneo mengine. Kama ndivyo, basi kupaka nakshi ya rangi tofauti na ile ya ukuta mzima huwa inaleta mvuto.
Vilevile kwenye kuchagua rangi ya nakshi  unatakiwa kuangalia mazingira mengine ya nje. Huenda maua, miti na ukoka umezidisha sana kijani. Unatakiwa kuchagua rangi ambayo itatawala hicho kijani.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755 200023

No comments:

Post a Comment