Pages

Monday, July 4, 2016

Mambo machache ya kuzingatia unapohitaji viti vya meza ya chakula

Unapohitaji viti vya meza ya chakula kuna njia mbili, ya kwanza ni kutengenezesha kwa mafundi na ya pili ni kununua vilivyo tayari ambapo mara nyingi hivi vinauzwa pamoja na meza yake.

Moja ya jambo muhimu unalotakiwa kufahamu ni kama unahitaji viti vilivyoshonewa vitambaa na
sponji au visivyokuwa na vitambaa na sponji. Yani kuna viti ambavyo kama ni mbao ni mbao yenyewe tu na kuna vile ambavyo kama ni vya mbao ni mbao pamoja na sponji na kitambaa kilichofunika hilo sponji.. Ni ukweli kuwa viti aina hii yenye vitambaa na sponji vinaonekana kuwa na mvuto na pia kuvikalia inakuwa burudani zaidi. Cha muhimu ni kuzingatia kuwa familia yako ina watu wa umri gani, kwa mfano meza ambayo inatumiwa na familia yenye watoto wadogo, vitambaa vya viti ni rahisi kuchafuliwa na kuharibiwa ndani ya kipindi kifupi. Kwahivyo unapaswa kujiuliza je, utaweza hiyo kazi ya kuvisafisha mara kwa mara? Kuna viti ambavyo havijashonewa sponji lakini vinakuwa na mito pembeni ambayo ni rahisi kubadilisha foronya na kusafisha wakati huohuo ukizingatia pia rangi ya kitambaa cha mito. Endapo una familia changa pengine hivi vya aina hii ndio vinakufaa zaidi ambapo utavibadilisha miaka ya mbeleni watoto wanavyokua wamekua wakubwa.

Jambo lingine la kuzingatia ni urefu wa viti vyako vya meza ya chakula. Huwa kuna tofauti ya urefu kwahivyo ni vyema kama unanunua meza kwingine na viti kwingine ujue kwamba viti unavyotaka kununua vinatosha kwenye meza uliyonayo. Pia kama viti vya meza ya chakula unavyotaka kununua vina mikono hakikisha kuwa haiko chini sana au juu sana kiasi cha kukuzuia kuwa karibu na meza pale unapokuwa umevikalia.

Jambo ambalo wengi wanaohitaji viti au walishapata tayari, hawajajua ni kwamba unaweza kuchanganya viti vya meza ya chakula toka kwenye vyanzo tofauti. Kwa mfano, viti vya mikono vinapendeza vikiwa viwili ambapo kila kimoja kinakuwa kwenye ule upande mwembamba wa meza. Viti hivi huwa vinafanya meza iwe ya kifahari kama navyo ni vya kifahari. Kwa maana hiyo kama meza yako ya chakula ni ya viti 6 kwa mfano, unaweza kununua hivi 4 vya gharama nafuu na vile viwili vyenye mikono ukanunua vya kifahari. Kuongeza hela kidogo zaidi ili kununua hivi viti viwili vitaifanya meza yote kuonekana ya daraja la juu!

Natumai dondoo hizi zitakusaidia wewe uliyeko kwenye mchakato wa kujipatia viti vya meza ya chakula.


Kwa ushauri njoo 0755200023

No comments:

Post a Comment