Kwa
siku za karibuni ukoka wa kutengeneza (artificial grass) umeanza kugusa mioyo
ya baadhi ya Watanzania, anasema muuzaji Saleh Ahmed wa kampuni ya Aqua Décor iliyopo
Kijitonyama simu 0712 792 909. Katika makala hii napenda wewe msomaji wangu uelimike kuhusu ukoka
huu endapo utavutiwa kuwa nao.
Ni
vyema ujue kwamba ni
muhimu ukoka wa kutengeneza unaotaka kununua uwe wa
kiwango bora na pia upate mtaalam wa usimikaji ambaye anaifahamu vyema kazi
hiyo.
Ukoka
wa kutengeneza wenye viwango vyote vya ubora utakupa faida nyingi zaidi ya
bustani ya asili ambapo faida moja kubwa ni kutokuhitaji kumwagiliwa. Ukiwekwa
vizuri ni hakika kwamba bustani yako mpya ya ukoka wa kutengeneza itaongeza thamani
ya nyumba yako huku ikiboresha maisha yako kwa kukupa eneo zuri la nje ya
nyumba la kuweza kukaaa kila wakati unapohitaji kufanya hivyo.
Ni
ukweli kuwa bustani kuweza kuwa ya kijani muda wote mwaka mzima ni gharama
kubwa. Ambao wanatumia ukoka huu wanafuraha jinsi maisha yalivyobadilika kuwa
mazuri kwani wanashangazwa na matokeo na faida ambazo hata mwanzo hawakuwa
wanazijua zote. Fikiria bustani ambayo hakuna kukatia majani tena, hakuna
kumwagilia tena, hakuna tope au mabaki ya majani yanayokuchafua miguu na pengine
hata kuingia ndani, hakuna kuweka mbolea na wala hakuna kupiga magoti kung’olea
magugu. Ukoka huu wa kutengeneza unaweza kukupumbaza kiasi kwamba ukadhani ni
ukoka hai. Ni mkombozi kwa walioko kwenye maeneo yenye ukame lakini bado
wanatamani kuwa na bustani isiyo na vumbi.
Kutokana
na mvuto wake unaweza kutamani kuvua viatu kabla hujakanyaga humo. Ukoka wa
kutengeneza ukiwa umesimikwa vizuri, hakuna jinsi unaweza kusema bustani ni feki kama hujaambiwa au kugusa. Ni
zulia la kweli la nje ya nyumba ambalo linaweza kudumu kati ya miaka 15 hadi
miaka 25 hivyo kukufanya uwe na bustani ya gharama nafuu sana ukilinganisha na
bustani hai.
Ni
eneo zuri la watoto kucheza.
Faida
zile zile zinazofanya ukoka wa kutengeneza kuwekwa kwenye baadhi ya viwanja vikubwa
vya michezo, na vilele vya majengo ya biashara sasa utakuwa unazipata moja kwa
moja nyumbani kwako.
Endapo
unataka kununua ukoka wa kutengeneza chagua ambao hauachi alama za nyayo au
viatu ukiwa umepita juu yake, ni rahisi kujaribu zoezi hili. Wenye ubora
unaokubalika huwa umewekwa kizuizi cha mionzi ya jua kwa hivyo usiogope kuwa rangi
ya kijani itachuja.
Wageni
watakaokutembelea bila shaka wataona wivu kwani huhitaji kumwagilia, ila bado
una bustani nzuri kushinda zao zilizokauka au zilizo chepechepe sana kwa ajili
ya kumwagiliwa maji mengi hasa wakati wa kiangazi kiasi kwamba hata kukaa
inakuwa ngumu.
Wewe unaonaje kuhusu ukoka wa kutengeneza, ni
mkombozi kwa wenye nyumba wapenda bustani
au sivyo?
No comments:
Post a Comment