Pages

Monday, November 21, 2016

Fremu ya mbao kwa ajili ya kitanda ni chaguo zuri zaidi



Naomba ingia instagram @mtotomagazine u like picha hii hapa chini ili ishinde. Asante sana


Moja kati ya maswali ambayo wengi wanaotaka kununua kitanda wanajiuliza ni kama wanunue cha mbao au cha chuma. Aina zote mbili zina faida na changamoto zake kama ifuatavyo.

Andrew Komba wa kampuni ya Furniture Mart iliyoko Tabata 
simu 0655 974 223 anasema kuwa fremu za mbao kwa ajili ya kitanda ni
imara na salama zaidi kuliko za chuma. Ni salama kwakuwa finishing yake haiachi ncha kali zinazoweza kuleta madhara ukilinganisha na cha chuma.

Kwa kawaida ya binadamu toka enzi, kitanda cha mbao kinampa mlalaji hisia za burudiko kuliko cha chuma, na pia kimapambo, kitengeneza mandhari ya kupendezesha chumba zaidi hasa kama kimetengenezwa kwa mbao ngumu na zenye rangi za asili. Mbao za mninga na mkongo zinakifanya kitanda kionekane cha kifahari na kinakipa chumba muonekano wa uhalisia, utulivu na ukamilifu.

Komba anasema, kitanda cha mbao ni bei nafuu ukilinganisha na ubora na uzuri unaotokana nacho. Usidanganyike kwa kutazama wakati wa kukinunua kuwa bei ni kubwa kwani ukweli ni kwamba kitanda cha mbao kinakupa garantii ya pesa zako hadi zaidi ya miaka 30 mbele. Ni kama umewekeza na ikitokea wakati wowote unataka kukiuza kutokana na sababu yoyote ile labda unahama mkoa, au unataka kikubwa zaidi ni kwamba thamani yake inaongezeka.

Kitanda cha mbao kinaweza kuwekwa urembo wa aina mbalimbali na pia kutiwa rangi kwa jinsi ambayo uzuri na michoro ya mbao bado inaonekana katika uhalisia wake. Au kwa mitindo ya siku hizi ambapo hupakwa rangi na kuleta muonekano na mguso tofauti kabisa kama vile tunavyoviona kwenye rangi nyeupe au nyeusi za mati. 

Kitanda cha mbao ni imara na hakina kelele kwakuwa mfumo wake wa kukifunga hautumii sukuruu za chuma ambazo hulegea baada ya muda mfupi.
Komba anasema kwa uzoefu wake na wateja wake ni kwamba kitanda cha mbao kina utulivu zaidi kwa usingizi ukilinganisha na kile cha chuma ambacho kinaweza kuwa na kelele na kisikupe usingizi mwororo, na pia fremu ya mbao inalifanya godoro litulie kitandani.

Ni rafiki wa mazingira, kwani unaweza kuitumia mbao hiyo tena na tena kwa manufaa mengine na pia miti inayotumika ni nishati mrudio ambayo inaoteshwa na kuota tena.
Kimuonekano vitanda vya mbao vinavutia na vina muonekano wa asili kwa sababu vinatengenezwa kutokana na miti ambacho ni kitu hai.
Ni rahisi kukitunza na kukifanyia marekebisho endapo kuna uharibifu umetokea.


Kutokana na uchambuzi huu ni matumaini kuwa itakurahisishia kufanya uamuzi pale unapotaka kununua kitanda, na kama ni cha mbao nunua cha mbao ngumu tofauti na cha bei rahisi kisichokuwa cha mbao halisi bali mabaki ya mbao. Vitanda vilivyotengenezwa kwa mabaki ya mbao baada ya muda vina hatari ya kuumuka na hasa pale vinapokutana na maji ndio mbaya zaidi, usidanganyike na muonekano wake wa kuvutia.

No comments:

Post a Comment