Pages

Monday, November 28, 2016

Njia 4 za kutayarisha nyumba yako kwa ajili ya sikukuu

Sikukuu za mwisho wa mwaka  na hatimaye mwaka mpya zinakaribia, na bila shaka wengi wetu tunajiweka tayari kwa sikukuu hizo.
Kuanzia kusafisha nyumba kila mahali toka mwaka uanze hadi kuweka mapambo ya sikukuu ni baadhi ya vitu vichache ambavyo tunafanya kila mwaka kuiweka nyumba tayari kwa sikukuu. Na hasa kama unaalika wageni.

Maandalizi haya yanachosha eeh? Hapana usichoke. Hapa ni njia nne za namna ya kutayarisha nyumba yako kwa ajili ya sikukuu bila nguvu au gharama kubwa hasa kama utaongeza mkono wa ziada kufanikisha zoezi hili.

 1. Fanya usafi wa kina ndani
Kama  ni muda mrefu toka uifanyie nyumba usafi wa kina, ni ukweli kuwa kutakuwa na utando wa vumbi kwenye maeneo kadhaa ya nyumba. Au hata zaidi ya kadhaa, huenda ni maeneo mengi tu, ila habari njema ni kwamba kuna kampuni nyingi zinazojishugulisha na ufanyaji wa usafi wa kina majumbani. Ambapo ni pamoja na kutumia mashine za upepo kusafisha mazulia viti na makochi, kudeki na kufuta vumbi na buibui. Na unajua hizo sehemu ndogo ngumu kufikika kila wakati? Kipindi hiki ndio wakati wake wa kuzifikia na kuzifanyia usafi. Tunazungumzia usafi wa sehemu kama juu ya fremu za milango, nyuma ya tanki la choo, nyuma ya sinki, chini ya makochi na hata kona za madirisha. Kila kona kufikiwa. Bila kusahau kufua kila kitu ambapo ni pamoja na pazia, matandiko, mazulia na kadhalika.

2. Safisha eneo la nje ya nyumba
Kwa uzuri ambao miti inaonekana, tunajua inaweza kusababisha ukoka ulio chini yake usiote vizuri au kuharibu paa kama ipo karibu nalo. Kabla ya kukaribisha sikukuu hakikisha unapruni miti hiyo ambayo huenda imefunga sana. Hii itafanya bustani na eneo la nje ya nyumba kuwa na mvuto. Kuendana na ukubwa na wingi wa miti uliyonayo bila shaka unaweza kumhusisha msaidizi mbali na mtunza bustani uliye naye. Hii ni njia rahisi ya kufanya hiyo kazi kwa haraka ikiwa ni pamoja na kuondoa majani na matawi yote aliyopunguza.
Ambapo kwa utaalam wake atasaidia pia kuondoa yale ya kwenye paa na kwenye mifereji ya maji ya mvua. Kwahivyo pamoja na hili zoezi la kupruni itajumuisha pia kukatia ukoka na maua yote kwa ujumla katika kuandaa nyumba kupokea sikukuu.

3. Paka rangi
Kuendana na hali ya rangi ya kuta za nje na ndani ya nyumba inaweza kukupasa kupaka mkono mmoja au miwili ya rangi. Kumbuka unapamba ndipo unasheherekea.

4. Weka mapambo ya sikukuu

Hapa ndipo wengi wanapopenda! Kutokana na utamaduni wa kila familia zoezi hili linaambatana na kupamba mti wa sikukuu, bila kusahau taa za vimulimuli.

Kujiunga Oriflame ni elfu 9 tu. Huhitaji hela nyingine ya kununua bidhaa na wala hatutembezi bidhaa. Unachopewa ni training na catalogue. Karibu 0755 200023

No comments:

Post a Comment