Pages

Tuesday, November 8, 2016

Njia rahisi na haraka za kuongeza dozi ya rangi ukutani

 
Ni rahisi kujisikia uchovu pale unapofikiria ni vitu gani unavyoweza kuleta ndani ili kuongeza dozi ya rangi kwa njia rahisi, haraka na gharama nafuu. Rangi inaongeza nguvu na uzuri wa ziada wa eneo, lakini cha muhimu ni kuamini jicho lako, kujiamini kwenye maamuzi yako, na usizidishe laa iwe unajaribu uone itakuwaje! Ladha zetu kuhusu rangi zinahama, zinaongezeka na zinabadilika mara kwa mara. Rangi fulani kwenye fenicha inaweza kuonekana ni ya kuvutia, lakini je
itakuwaje unatapotaka kubadilisha rangi za vitu vingine kama vile pazia, kuta na kadhalika huko mbeleni? Kuongeza dozi ya rangi kwa kutumia vitu na kazi za sanaa ni rahisi na wigo ni mpana.

Uzuri ni kwamba vitu na kazi za sanaa zinaweza kuhamishwa kutoka chumba hadi chumba pale unapoamua kwenda na mtindo mwingine. Usumbufu wa kuhamisha si mkubwa na vilevile bei huwa si za kutisha ukilinganisha na mfano wa zoezi la kubadilisha rangi ya ukuta, au kubandua wallpaper ili kubandika nyingine.

Njia ya kwanza ya kuongeza dozi ya rangi ukutani ni kwa kutumia sanaa, vitu au mapambo madogodogo. Sehemu ikiwa na mwanga sahihi na unajitahidi kuongeza dozi ya rangi, hebu fikiria picha za ukutani zenye fremu nyeusi na nyeupe. Changanya picha zako hizo na nyingine mbili au tatu zenye rangi tofauti, kama unataka rangi za kuwaka fikiria sanaa zenye kazi nyekundu, chungwa, pinki, njano, bluu na kijani.  Na hapo itategemea na ukali wa rangi unaohitaji. Kumbuka rangi zote hizi nilizotaja zina familia ambapo kuna ukali wa kiwango tofauti tofauti kuanzia zile nyepesi hadi nzito.

Kuna hii njia nyingine ya kutumia sanaa chache kubwa endapo kuchagua rangi kwa sanaa ndogondogo kunakupa shida. Kwa njia hii unaweza ukachagua kitu au sanaa moja au mbili kubwa za rangi ili kuzitundika kwenye kuta zenye rangi nyepesi. Kuongeza sanaa moja au mbili zenye rangi nzito kuendana na ukubwa wa ukuta itasaidi kutengeneza eneo la kitovu kama unafikiria kuhamisha jichoi kutoka kwenye sofa, fenicha nyingine kubwa au luninga.

Njia ya tatu ni kwa kuchagua rangi zinazopishana. Hii ni kama kuanzisha mazungumzo kati ya sofa, meza ya kahama, au maua ya kona na ukuta. Ni kutafuta vitu vya rangi mbalimbali ndani ya nyumba yako ambavyo vinasaidia kutengeneza mpishano wa rangi katika sehemu tofauti za chumba na sehemu ya ukuta. Kuchanganya rangi kwa namna hii kunasaidia kuongeza utajiri wa rangi na hivyo kukamilisha dozi.

Hata kama umebandika wallpaper, bado unaweza kuongeza vitu va rangi ukutani kwa kuhusisha maua na michoro iliyoko kwenye wallpaper hiyo.

NIFUATE INSTAGRAM @vivimachange

No comments:

Post a Comment