Pages
▼
Tuesday, March 28, 2017
FAIDA ZA UPIMAJI NA UMILIKI ARDHI (Viwanja na Mashamba)
Surveyor James Aloyce
-Je kuna faida yeyote mwananchi anaweza kuipata endapo ataipima na kumiliki ardhi yake?
Jibu ni ndio mwananchi anaweza akapata faida pindi atakapopima na kumiliki ardhi yake kisheria
-Faida hizo ni zipi anazoweza pata mwananchi huyu aliepima na
kumiliki ardhi kisheria?
1. Utambuzi wa kisheria kuwa yeye ni mmiliki halali wa kipande hiko cha ardhi.
2. Kuongeza thamani ya ardhi yake, ukipima na ukamiliki kisheria ardhi yako inapanda thamani kwa kuwa umiliki wako unatambulika kisheria.
3. Kuongeza usalama katika ardhi yako, hivyo kuzuia mtu yeyote kujimilikisha au kufanya shuguli yeyote katika ardhi yako bila ridhaa yako.
4. Kutumika kwa hati miliki yako kama dhamana katika uombaji wa mikopo benki na taasisi za kifedha. (Hivyo inaweza kukuinua kiuchumi)
5. Kuondoa migogoro na majirani zako na pia usumbufu pindi unapotaka kuiuza ardhi hiyo.
Hivyo pima ardhi yako na umiliki kisheria kwa usalama na maendeleo ya baadae
By Surveyor James Aloyce
0713778937
No comments:
Post a Comment