Pages

Thursday, May 18, 2017

Muongozo wa maumbo mbalimbali ya vyandarua

Kutokana na uwepo wa vyandarua vya maumbo na uwekaji wa aina nyingi inaweza kukuchanganya kwamba ni kipi sahihi kwako.Usihamaki! Hapa nitakupa muongozo wa kile unachotakiwa kufahamu kwa baadhi ya maumbo maarufu zaidi ya vyandarua vya kisasa sokoni.

Naamini muongozo huu utakusaidia kuchagua chandarua sahihi ili usiendelee kutafunwa na mbu ukiwa bado hai! Kama unachanganyikiwa na vyandarua vya umbo la
kengele, boksi, vya kuchimbia darini au ukutani au hata vyenye eneo moja la kuingilia au maeneo manne au hakijapasuliwa kabisa na kadhalika karibu ujielimishe

Vyandarua vya kujitegemea
Vyandarua vya kujitegemea ni aina ya nyandarua ambavyo vina fremu zake ambazo aidha ni bomba za chuma, plastiki au aluminiam ambapo vinashikilia godoro na neti kama vile hema. Havihitaji sehemu yoyote ya kuning’inizwa na vina zipu kiasi kwamba mlalaji ukiwa umelala unakuwa umejifungia kabisa ndani.

Faida za vyandarua vya muundo huu ni uwekaji wake ambao ni rahisi, huhitaji ngazi, kulabu , kutoboa wala fundi. Vinaweza kutumika popote ndani kitandani au varandani sakafuni. Mazingira yake ya ndani ni salama zaidi kwa watoto wadogo n wachanga, kinasaidia kumkinga asianguke hata pale anapojigeuza.

Changamoto yake ni kwamba kwa ajili vina fremu za kukishikilia vinachukua nafasi hasa pale unapotaka kusafiri nacho mbali tofauti na vile vya kutundika darini visivyokuwa na fremu. Mabomba yake hayajikunji kirahisi.Fremu yake ikiharibika inaweza kuwa changamoto kuifanyia marekebisho. Vinafaa zaidi kwenye vitanda vidogo kwani hata utandikaji unakuwa rahisi kwa ajili kumbuka kuwa godoro linaingizwa ndani ya chandarua. Huwezi kuketi kitandani wakati wa mchana kwa kuning’iniza miguu.

Vyandarua vya umbo la kengele
Hivi ni vile vyandarua vyenye umbo kama la kengele. Ni vya kale zaidi ambapo vina pointi moja tu ya kutundika kwa kulabu ya darini. Eneo la juu ni jembamba na chandarua kinatanuka kadri kinavyofikia matandiko. Faida ya vyandarua hivi ni kwamba ni gharama nafuu. Ni rahisi kukiweka na kukiondoa hasa wakati unapohitaji kukifua. Ni rahisi kufungasha wakati unapotaka kusafiri nacho. Vinaweza kutumiwa kwenye vitanda mbalimbali kuanzia vile vidogo vya watoto wanaosoma shule za kulala, vitanda vya hosteli na vikubwa vya nyumbani.
Changamoto yake ni kwamba vingi ni vyembamba ambapo kuchomekwa na uchomolewa kila wakati vinakifanye kiwe rahisi kuchanika. Inahitajika kuwe na kulabu na dari imara.

Vyandarua vya umbo la boksi
Vyandarua hivi ni vya kisasa zaidi. Vina umbo la boksi ambapo vinafiti kwenye kitanda chote na vinasimikwa aidha kweye kona za kitanda, ukutani au darini kwa pembe zote nne. Vina bomba zake maalum za kutengeneza huonekano huo wa umbo la boksi. Huwa vina urembo wa kuzunguka chandarua na hivyo vinakuwa ni kama pambo chumbani. Vinatakiwa kutumika ndani ya nyumba na kwa sehemu ya kudumu kama vile chumba cha kulala, hospitalini au hotelini. Vipo vyenye kamba ya kukifungua na kufunga na kupitia reli za fremu au kwa staili ya kupandika na kushusha.
Faida za vyandua vya boksi ni uhuru wake katika matumizi ambapo vina nafasi kubwa kuliko vingine vyote.
Changamoto zake ni kwamba huwezi kukifunga mwenyewe, ni lazima umhusishe fundi. Vilevile ni ngumu kukifungua unapotaka kukifua kama hujaonyeshwa na fundi namna ya kukitoa. Hii ni kwasababu kimeuganishawa kwenye maeneo mengi kutokana na fremu na ukubwa wa chandarua hiki. Watoto wanapenda kuvuta kamba zake wakati ambapo hakitumiki. Kumbka kuziweka kwa juu zisining’inie ili wasiweze kuchezea.

Msomaji wangu, ni vyema kufahamu ukubwa wa mahali unapotaka kuweka chandarua kwani feni au taa darini vinaweza kuleta kikwazo. Nina hakika umepata mwanga kuhusiana na aina mbalimbali za vyandara zilizopo sokoni.


Kwa mahitaji ya neti toa oda yako 0755 200023.

No comments:

Post a Comment