Pages

Thursday, July 6, 2017

TANZIA:....Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia

Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu kwa takriban wiki mbili, mwanaye Hamad Dede amethibitisha.

Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es Salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitakapokamilika kupangwa.

No comments:

Post a Comment