Pages

Monday, September 25, 2017

Gauni la mgongo wazi / Backless dress

Gauni hili lipo kwenye rangi hizi 2. Bei 60,000
Tupo Sinza Kamanyola
Tunatuma popote
Mawasiliano 0755200023

Kutoka: mwanaspoti.co.tz
KILA kukicha mitindo mpya inazuka, kuna watu hudandia mitindo fulani bila kufahamu wanatakiwa wavae nguo za aina hiyo kwa wakati gani. Hebu tuangalie mtindo wa mgongo wazi 'Backless Dress' unavaliwa namna gani. Jambo la kwanza la kuzingatia kwa mvaaji, ni kuhakikisha kwamba unavaa nguo hiyo ukiwa na 'mtoko' wa jioni na wala si kuvaa nguo hiyo wakati wa mchana na kuzurula nayo mitaani.
Ukivaa nguo ya aina hiyo na kutua nayo ofisini watu watakushangaa. Jambo jingine la kuzingatia ni kuhakikisha mgongo wako hauna mikunjo ya nyama, yaani 'minyama uzembe'. Mikunjo hiyo kwa kawaida huwa haipendezi mbele ya macho ya watu. 

Kama unaona kwamba hali yako ipo hivyo tafuta nguo nyingine. Vile vile mtindo wa 'Backless' unavutia wakati mtu anapokuwa hajavaa sidiria au iwapo amevaa sidiria maalum ambayo hukusanya matiti kwa mbele. 

Ikumbukwe kwamba sidiria inapoonekana mtu havutii. Mhusika pia anatakiwa kupaka mafuta mpaka mgongoni ili asipauke na kugeuka kichekesho. Mgongo uliopauka haupendezi. Vile vile epuka kuvaa nguo ya mtindo huo wakati wa baridi kali kwani unaweza kupata maradhi hasa kichomi na mengineyo.


No comments:

Post a Comment