Pages

Saturday, July 8, 2023

CCM Imemfukuza Uanachama Balozi Ali Karume



Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kusini Unguja imemfuta uanachama kada wake Balozi Ali Karume.

Taarifa ya kumuondoa kwenye chama imetolewa na katibu mwenezi wa mkoa huo Ali Timamu Haji kutokana na kikao kilichofanyika saa saba usiku wa kuamkia leo julai 8, 2023 chini ya Katibu wa CCM wa mkoa Amina Mnacho.

Hatua hiyo inakuja baada ya CCM kumpa onyo kutokana na kauli zake akidaiwa kukidhalilisha na kuwatukana viongozi wakuu hadharani.

Nifollow so @ViviMachangeBlog

Tangaza Biashara yako hapa wasiliana na 0755200023

No comments:

Post a Comment