Pages

Wednesday, September 4, 2013

Jinsi ya kurahisisha maisha: Nyumba ya wafanyakazi

Mpendwa msomaji wangu,

Ninapenda mno kuyafanya maisha yawe rahisi. Kwa hivyo nimeamua kuwa nitakuwa naandika dondoo za jinsi ya kurahisisha maisha na kwa leo naanza na umuhimu wa kuwa na nyumba ya wafanyakazi. Kwenye dondoo hii nyumba ya wafanyakazi nitaiita servant quarter na kwa ufupi SQ. 
SQ ni maarufu kwenye nyumba kubwa na inaweza kuwa ni nyumba ndogo ya uani au basement. Kwa wenye nyumba wengi SQ imekuwa overlooked ingawa kiukweli inasaidia mno mno. Kama unayo kwenye makazi yako utashuhudia hili ninaloandika. 

Kihistoria ni kuwa SQ ilikuwa utamaduni wa wenzetu walioendelea lakini kutokana na faida zake hata sisi tunaoendelea tukaiga. SQ itakusaidia kuwa na destination kwa wafanyakazi waliopo kwenye makazi yako iwe ni walinzi, gardener, hausigeli na wakati mwingine hata mgeni atakayekutembelea. Kwa mfano unajua jinsi hausigeli wanavyokuja na kukimbia; huna haja ya kuwaambukiza watoto wako harara! Wafanyakazi wote hawa watakuwa na sehemu ya kulia chakula, kulala ama kubadilisha nguo na hata bafu na choo bila kukupa usumbufu wowote ama kukuvuruga wewe na familia yako. SQ itakupa faragha wewe na familia yako. Ukisafiri na familia yako unafunga nyumba yako kubwa maisha yanaendelea kama kawa ndani ya SQ. Ni uhuru ulioje! Nikitembelea makazi yoyote na kukutana na SQ natamani kuibusu kwa jinsi inavyorahisiha maisha. 


Kama unajenga nyumba ya kuishi leo tafadhali sana kumbuka SQ, hata kama uliisahau lakini bado una nafasi kwenye makazi yako ijenge leo na utarudi hapa kushuhudia faida zake.

No comments:

Post a Comment