Pages

Monday, September 16, 2013

wengi wamevutiwa na ujasiriamali

kutokana na pilika na mishemishe sikukumbuka kuwa kipindi nilichohojiwa kimerushwa jana. nimeshangaa leo napata sms na simu nyingi za pongezi na maswali toka kwa wasikilizaji, ambao ndio wameniambia kuwa walinisikia hewani. wananiuliza mwenye simu hii ndio alikuwa anaongea? wengi niliowauliza wamevutiwa na nini kwenye mahojiano yale wananiambia kuwa wamevutiwa na kipengele cha ujasiliamali. ha ha haaa..kuna mahali nilichombeza eti mafanikio yangu ni kumsaidia Raisi Kikwete kuongeza ajira kwani ndani ya mwaka mmoja na ushee wa ujasiriamali nimeweza kuajiri watu 10! na vitu viwili vikubwa ili uweze kuwa mjasiriamali ni kuwa na plan na resources. vitu hivi viwili tu vinakutoa...unaanza kidogokidogo ukisha gain momentum unachochea! karibuni kwenye ulimwengu wa ujasiaramali!

tunaosha magari

tunaosha mazulia

tunafanya laundry & dry cleaning, nikiwa nanyoosha mgongo baada ya kunyoosha nguo za wateja        

No comments:

Post a Comment