Pages

Thursday, October 31, 2013

My article for newspaper: Fenicha za chumba cha chakula

Kuwa na chumba cha kulia chakula katika eneo lolote la nyumba yako ni baraka. Kuwa na chumba cha kulia chakula chenye ukubwa wa kutosha kuweka fenicha zinazotakiwa kuwa kwenye chumba hiki ni ukweli kuwa itakuwezesha na kukuongezea ubunifu wa kupamba ndani mwako.

Fenicha za muhimu zaidi zinazotakiwa kuwa katika chumba cha kulia chakula ni meza na viti vyake, lakini hata hivyo kama una nafasi ya kutosha unaweza kuweka kabati la vyombo kwa ajili ya matumizi na mapambo.  Mapambo kwenye chumba cha kulia chakula yawe machache sana ili kuondoa mrundikano na kuacha sehemu kubwa ya familia.

cha chumba cha kulia chakula ni meza, ichague kwa uangalifu kutoka za pembe nne, duara au yai. Amua kama unataka ya viti vinne, sita au nane. Kimsingi umbo na nafasi ya chumba cha kulia chakula lazima itizamwe kabla ya kuamua umbo la meza inayotakiwa kuwa hapo. Isiwe kubwa kiasi ambacho itadumaza eneo la chumba wala isiwe ndogo kiasi ambacho itazama ipotelee.

Fikiria ni viti vingapi unahitaji kwenye meza ya chumba chako cha kulia chakula, mara nyingi ukweli huu utategemea na aina na ukubwa wa meza utakayonunua. Kama unajisikia kuwa viti vinne vitakidhi hitaji lako, fikiria meza ya duara au pembe nne. Pia fikiria kama utahitaji vile viti vyenye mikono kwenye meza yako ama laa; unaweza hata ukaamua kuchanganya hapa; weka viti vya mikono kwenye pande zile fupi za meza zinazotizamana halafu vile visivyo na mikono weka pande ndefu. Pia fikiria urefu na uzito wa viti, vinatakiwa kuwa na urefu na upana wa kutosha kwa ajili ya kukaa na kujisikia burudani na wakati huo huo visiwe vyepesi ili visisogee sogee kila mara.

Kama umebahatika kuwa na nafasi ya kutosha kwenye chumba chako cha kulia chakula weka kabati la vyombo. Makabati ya vyombo ya kwenye chumba cha chakula yako ya aina nyingi mno, lakini karibu yote yana milango ya vioo na mashelfu kwa ajili ya kuona kirahisi vilivyomo.  Kabati la vyombo katika chumba cha kulia chakula lina faida tatu ambazo ni sehemu ya nyongeza ya kuhifadhia vyombo vyako hasa vile ambavyo ni maalum na vinatolewa kwa matukio maalum na kwa wageni maalum. Pili, ni mahali pa nyongeza pa  kupakulia chakula hasa wakati unapoburudisha, unaweza ukahifadhia vinywaji na pia nafasi ya kuweka bufee na saladi na hata baadhi ya vitafunwa. Tatu ni mahali utakapoweza kuweka mapambo yako. Unaweza kuonyesha mapambo yako ya kichina, vyombo vya glasi na hata kuhifadhia vitambaa vya meza ambavyo havitumiki kwa wakati huo. Kumbuka kuwa makabati haya yanaweza kubuniwa kuendana na eneo unalotaka kuweka na matamanio yako.

Wakati hakuna njia mbaya au nzuri ya kupanga vilivyomo ndani ya kabati la vyombo la kwenye chumba cha kulia chakula; kuna njia za kimkakati za kupamba ambazo zinaleta mvuto. Kusanya vifaa vyote unavyotaka kuweka kwenye kabati na vipange mbele yako sehemu tambarare. Nyanyua kimoja kimoja upange vifaa vinavyovutia zaidi iwe ni vya glasi, kioo au seramiki kwenye shelfu la kabati lililo usawa na macho yako. Vifaa vikubwa vianze kwa ndani karibia na kuta na vile vidogo vipange karibia na mlangoni.
Vifaa vilivyobakia vipange kwenye mashelfu mengine kwa mtiririko huo huo wa hapo juu. Ongeza baadhi ya vifaa ambavyo kwa namna fulani vipo nje ya kawaida, lakini bado vina mvuto. Hii itafanya muonekano wa kabati lako uvutie. Kwa mfano, picha ya fremu ya wanafamilia inafaa, au mpira au mdoli wa kuvutia, utafanya ule mpangilio wako uwe na mvuto. 

Ongezea vifaa vya msimu kulingana na majira ya mwaka. Kwa mfano, kama ni karibia na krismasi weka mapambo machache kwenye shelfu au karibia na siku ya wapendanao weka kadi nzuri za valentine kuongeza mguso wa rangi kwenye kabati lako.

Sanaa chache za maonyesho zilizochaguliwa, na mwanga wa kuvutia vinaweza kuwa ndio mapambo machache tu ambayo chumba chako cha kulia chakula kinahitaji. Kama kuta zinaonekana kuwa tupu zivalishe kwa fremu za picha za maakuli lakini hakikisha unaweka chache sana kuondoa mrundikano kwenye chumba hiki. Zaidi ya yote chumba chako cha kulia chakula ni kijiwe chako na familia yako kutumia muda wenu wa thamani pamoja.

Kumbuka ili utumie hela yako kwa busara, wakati wa kuchagua fenicha za chumba cha kulia chakula, unapaswa kuwa makini na vigezo vikuu vitatu. Kwanza ni zingatia umbo, ukubwa na vipimo vya chumba au hapo mahali pa kulia chakula, na pili mandhari unayotaka kutengeneza kwamba ni ya kimapumziko, kitamaduni, rasmi na orodha inaendelea, tatu ni idadi gani ya viti unayotaka meza iwe navyo na mwisho ni aina ya mapambo ambayo unadhani chumba kinahitaji. Kutegemea na nafasi na pia mahitaji binafsi, amua ni fenicha zipi hasa unahitaji kwa ajili ya chumba chako cha kulia chakula.
 
Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi ni mjasiriamali upande wa usafi wa mazulia, nguo na magari; pia ana mapenzi makubwa ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk



Monday, October 28, 2013

kazi hizi za mikono ni murua kwa mapambo ya ndani

hapa hiki kimkeka cha duara kimepamba ukutani

hapa kimkeka kimepambwa mezani

hii ya mahanjumati waweza ipamba kwenye ukuta wa dining room

msingi wa kweli wa ndoa huu hapa

ama kweli kuna watu wanakaa na kufikiri..."living for the first love".imenikumbusha pambio..upendo ule ule, upendo ule wa kwanza...kamwe usibadilishe

Friday, October 25, 2013

wavijua hivi...

kwenye udongo laini ili usiharibu kisigino chembamba cha viatu vyako, tuseme umealikwa kwenye kimnuso cha bustanini vaa vidude hivi. vinapatikana deshi deshi..

Thursday, October 24, 2013

colorful view

start your thursday with "no hard feelings"....

Wednesday, October 23, 2013

huyu ni nani?

kama kuna samaki mtu basi na huyu kwa haraka naweza sema ni simba mtu..

worry not..

nilipo blog kuhusu hili sanamu nilipata comments za kuchekesha sana. hilo hapo sasa limeshajengewa nyumba


My article for newspaper: Muonekano wa bustani mahali ndoa inapofungwa






Apa kiapo cha ndoa yako mahali pa kipekee na pa kumbukumbu maishani kwa sababu unastahili. Kwa kawaida ndoa zinafanyika, nyumbani kwa ndoa za kimila ama kwenye nyumba za ibada ama kwa ofisi za msajili wa ndoa wa serikali. Ila kwa siku za karibuni kutokana na utandawazi dunia imekuwa kijiji kwa hivyo kusababisha walimwengu kuigana tamaduni hasa zile ambazo jamii husika inaona zinafaa. Eneo mojawapo lililoathirika na utandawazi ni hili la mahali pa kufungia ndoa. Ndoa za kufungwa kwenye bustani au maeneo mengine kama ya makumbusho na vivutio vingine ni jambo linalokuja kwa kasi na ni tamanio la mabibi harusi wengi.

Harusi inaweza kuwa ndilo tukio maalum kuliko yote kwenye maisha ya mtu. Ni tukio la maajabu na hata hivyo linaweza kuleta msongo wa mawazo hasa kwa muoaji na muolewaji ila siendi kuongelea hilo kwa sasa. Tunaenda kuangalia muonekano wa eneo la bustani ambapo ndoa itafungwa namna ya kulifanya lionekane maridadi kuwa na mpangilio hivyo kufanya tukio la kufunga ndoa yako kuwa la kipekee kuanzia pale wanapokaa viongozi wa kufanga ndoa, bwana na bibi harusi hadi kwa wageni waalikwa.

Kila bibi harusi mtarajiwa anachagua rangi za harusi yake kutokana na matakwa yake binafsi, lakini kupamba kwenye bustani inamaanisha kuwa asili imeshakufanyia nusu ya kazi yako! Ni kama umeshapewa bonasi ya mapambo kwa ndoa inayofungiwa kwenye bustani ila hata hivyo bado unatakiwa kufanya kazi kidogo. Tembelea bustani husika wiki moja kabla ya harusi kuhakikisha kuwa majani yamekatwa, chini kumerekiwa na maua yamekatiwa. Kama kuna upungufu wa maua labda ni kipindi cha jua kali hakikisha unaongeza hata kama ni ya vyungu toka kwa wauzaji.
Kama mmeamua kuapa kiapo chenu cha ndoa kwenye bustani kuna mawazo lukuki ya jinsi ya kufanya eneo hili livutie kwa wageni na kwa picha zenu za kumbukumbu kwa siku hiyo kubwa!
Kwanza kabisa angalia hapo mahali kama kuna kitu cha asili kama vile mti. Kwenye eneo hili ndipo utakapoweza kuweka kijukwaa kwa ajili ya viongozi wanaofunga hiyo ndoa. Na unaweza kuninginiza mapambo kwenye mtio huo vile vile. Leo, zaidi ya ilivyowahi kuwa, kijani cha bustani ni pambo tosha, usichezee hela kununua maua mengi ya ziada, tumia vitu vya asili vilivyoko eneo hilo hilo la bustani. Chagua mapambo machache sana ya rangi ambazo zitaendana na zilizopo kwenye bustani asili tayari, badala ya kuchagua ambazo zitashindana nazo.

Baada ya hapo panga viti vya mashuhuda/wageni watakaofika kushuhudia mkifunga ndoa. Tumia viti vya kuvutia kwa rangi na staili zinazokubaliana na mandhari yako. Viti vingi vya bustanini ni vya chuma  na mbao ambavyo vinaweza kuwa sio burudani kwa kaa kwa muda. Ukiweza kutupia mito ya viti itakuwa bora zaidi na pia inaongeza mguso wa mapambo.

Kwenye hivi viti panga vikae mpangilio wa pande mbili kwa maana ya kuacha njia katikati ya pande hizo. Kwenye viti vya mstari wa  pembezoni mwa njia unaweza kupamba kwa kuvifunga tai na maua. Kama ni eneo lenye jua kali sana hakikisha mpambaji wako anatayarisha maua lakini ayafunge dakika chache kabla ya tukio kuanza ili yasinyaukie juani.

Kwenye njia iliyoko kati ya pande mbili za viti acha uzuri wa asili wa majani ya bustani, huna haja ya kutandika zulia kwenye njia hii. Badala yake kwa kusaidia viatu wa bibi harusi na wageni wengine waliovaa viatu vya kisigino chembamba kinachoweza kuchimba chini kutokana na udongo laini wa bustani weka mawe ya kukanyagia kama yale ya Tanga ambayo yana kawaida ya kuonekana kwenye bustani kwa hivyo nayo ni kivutio. Pia weka mahali pa kuingilia kwenye eneo hili la bustani lililotengwa kwa shughuli na papambe.

Fikiria hali ya hewa na muda. Si busara kukaanga wageni wako kwenye jua kali kwa mfano. Chagua muda ambao jua sio kali kwa kuwa hutaki kuweka kivuli kwa ajili unataka uzuri wa asili wa bustani. Pia ni vyema ukatenga eneo la mbali kidogo hapo hapo bustanini kwa kuweka paa endapo una wasiwasi wa mvua kunyesha. Na hakikisha wale wageni wanaotoka mbali na hawajui hali ya hewa ya eneo husika unawataarifu kabla. Wengine wanapenda kupaka yale mafuta ya kuzuia jua.

Weka alama za kuelekeza wageni. Bustanini panapofungwa ndoa panaweza kuwa ni mbali toka wageni wanakoshukia, labda kwa mbele kuna jengo kwa mfano na bustani ipo nyuma ya hilo jingo. Inabidi kuweka alama za kuwaonyesha wageni wako eneo bustani ilipo. Vibao vyako vya kuelekeza vinaweza kuandikwa pia lugha ya wageni wako wengine ambao hawajui lugha kuu ya hapo kama wapo. Kwa mfano inawezekana kuna wageni wasiojua Kiswahili, hakikisha  umewawekea lugha yao nao wajisikie wapo nyumbani. Vibao hivi visiwe tofauti na mandhari nzima ya rangi zako za harusi ulizochagua.

Je kila mtu anaweza kusikia? Kama ukipiga picha ya ndoto yako ya kufungia ndoa kwenye bustani karibia na bahari pata picha upepo na kelele za watoto wanaocheza ufukweni. Usisahau kipaza sauti mahali pa kufungia ndoa. Mtu wako wa mziki ataweza kukusaidia katika hili.

Yote kwa yote kumbuka kuwa ndoa ni cheti! Hakikisha taasisi zinazohusika zinakubaliana na ndoa kufungiwa eneo ulilochagua.
Kama umeamua kufungia ndoa kwenye bustani, hongera! Ndoa hizi zina mahaba na ni nzuri. Nakutakia safari njema ya hatua inayofuata ya kuelekea kwenye sherehe ya harusi.

Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi ni mjasiriamali upande wa usafi wa mazulia, nguo na magari; pia ana mapenzi makubwa ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk

morningwood..

napenda napenda napenda sunrise, yani ile naamka na kigiza halafu naliona jua lileee linanyanyuka. hapo ndio mchakamchaka unaanza na linavyozidi kukomaa ndio siku inavyo slow down.
mwezi huu jua linachomoza mapema sana saa kumi na moja na nusu tayari. 
nachukia kuamka nikute tayari limeshakomaa yani naona kama siku yangu imedoda kwani sisi wachagger tunasema biashara ni asubuhi jioni kuhesabu pesa. sipendi sunset kama ninavyopenda sunrise!
sunrise

kijua kinaanza kupiga piga baadhi ya maeneo

Monday, October 21, 2013

majani kipenzi cha watoto..

yani watoto wakijua kwenye bustani yako kuna mmea huu utakoma. hawatakauka kuja kwako, wanayapenda haya majani ni laini basi wanang'ofoa na kuchezea.. utoto kweli raha.. halafu ukienda kwa rafiki ukiona ua lolote haliko kwenu basi lazima uliombe ukaoteshe kwenu pia...jamani..watoto wa sasa wa dot com wanakosa mengi. kumbuka mtoto ni chini ya miaka 18. lol

Saturday, October 19, 2013

jumba la MJ huko Chicago liko tayari kuingia sokoni

twende hatua kwa hatua tuvinjari baadhi ya vyumba vya jumba hilo la mkongwe Michael Jordan linalouzwa
getini

muonekano wa mbele

jiko

Sebule

MJ mwenyewe
picha kwa hisani ya yahoo

Friday, October 18, 2013

njia za kuboresha bafu lako

huwezi kukataa kuwa bafuni ni sehemu moja ndani ya nyumba ambayo inasahaulika. hata kama tunatumia muda mwingi hapo, ni rahisi kutoka kufunga mlango na kupasahau. lakini hivi karibuni nimekutana na post ambayo imeeleza jinsi rahisi ya kuboresha bafu lako.

jambo la kwanza ambalo limependekezwa ni kubadilisha taulo, vizulia na pazia kulipa bafu muonekano mpya. pia jaribu kubadilisha bomba lolote lenye kutu kwa mfano lile la mvua. ingawa hata kama utabadili pazia na kuweka taulo mpya kama vifaa vyako vya urembo vimetupwatupwa kila mahali vitalipa bafu ukakasi.
 vitu vyako vya urembo ambavyo unataka ukinyanyua mkono tu unachukua viweke pamoja itasaidia kuokoa muda na kufanya maeneo ya sinki yawe safi
kuwa na vifaa vya lazma vya usafi bafuni kama vile windex kwa ajili ya kusafishia kioo, harpic kwa kusafishia choo na vim kwa kusafishia sinki
tupa vifaa vilivyoisha muda wake na pia tosa vile ambavyo hutumii. kwa mfano utakuta kila ukinunua dawa ya meno kuna mswaki mpya, kwa hivyo usipokuwa makini unaweza kuwa na miswaki lukuki imezagaa
karatasi za chooni sio kitu maridadi cha kuonekana onekana hovyo, ila ni kitu muhimu sana. badala ya kusema uhifadhi stoo wakati ambapo huwezi kuzipata kirahisi wakati wa kutumia, weka chache ndani ya kikapu au ki bin maridadi. namna hii itaonekana nadhifu na rahisi kufikika.
hifadhi taulo za mgeni. kama hakuna mgeni kwa nini ujisumbue kuweka taulo maalum. weka bafuni zile ambazo unatumia na hizo na mgeni hifadhi mahali pengine.


Thursday, October 17, 2013

nyumba ya vioo nyingine hiyo..huenda tukajakutana na nyumba ya milango tu!


wenyewe wakiwa ndani wanajivinjari

inavyoonekana usiku

Plenty of natural sunlight isn't an unusual quality of a dream home. But what about a home built completely of glass so the light would never be hidden? For a pair of young artists, a beautiful sunset and a thoughtful conversation led to the construction of a breathtaking retreat in mountainous West Virginia.

Early on in their relationship, Olson invited Horwitz to join him on a trip to his family’s property in southern West Virginia. One evening, the two went on a walk in the woods that resulted in an artistic vision.
As the sun sank behind a hill, the couple began talking about how amazing the light appeared at that moment. What if, they pondered, there could be a living space where light changed based on the time of day?
“Light is so different in the morning, at noon and at dusk. We wanted to somehow build a house so that change happened in our living space,” Olson said. “It’s about being closer to living with the elements.”

Both Olson and Horwitz had summer plans to work at their current jobs, but agreed they had suddenly discovered a project worth pursuing.
In what Olson calls a “spur-of-the-moment decision,” the new couple quit their jobs, rented a U-Haul and began driving state to state to find the right windows for a home made completely of glass.
The couple's unique cabin was featured in "Half Cut Tea," a Web video series that explores artists and their works. (Their episode is at the bottom of this blog post.) Olson is friends with one of the series creators, Jordan Wayne Long, a performance artist originally from Bald Knob, Arkansas, who interviewed the couple and showcased their home.

Most of the windows the couple collected were found or scavenged, Olson said. Some were purchased, but not many. The first the couple found was in a big stack of old windows at an abandoned barn in Pennsylvania. Horwitz describes finding that window as “serendipitous.”
When they had collected enough glass, the two began constructing the home on the family land near New River Gorge National River park. The closest town to the property is Hinton, West Virginia, Olson said.
The building process was sometimes frustrating, Horwitz said. The two built the entire structure themselves – their only audience was the occasional curious deer, rabbit or fox. The home’s front window wall is about 16 feet high, but the base of the structure is another 4 feet off the ground, Horwitz said.
“It was just the two of us trying to put up these gigantic posts. It was scary and hard,” she said. “Looking at it now, it’s just totally insane. It’s huge. I realize now that’s what makes it so amazing.”

Olson credits an artistic vision and frugality with the success of the home. While living on a diet of rice and beans, the two used nails, wood and anything salvageable from an old barn on the property to piece their enormous structure together. They estimate they spent $500 in total on the project.
“Even the roofing we took from the abandoned barn,” Olson said. “We were able to make it a reality because we are first artists and creators. We had to be resourceful to do it cheaply.”
After months of work, the home was completed in December. On what was once a pile of old windows and a patch of wooded land stood a beautiful glass building. Though there is no plumbing or electricity, the two artists said they enjoy the space as an escape.

described her favorite time of day inside the home as the “nighttime sun” – just as dusk falls.
“That’s when everything inside is on fire,” she said.
Olson said he’s awestruck after the sun goes down.
“The house is an experience at night,” Olson said. “The fireflies start at the ground and merge to the stars up above. It’s really like you’re sleeping under the stars.”

Someday Olson and Horwitz hope to build onto the home and add an outdoor kitchen, solar power and a wood-burning stove, they said. But for now, the Milwaukee-based couple said, they’ll enjoy the home as a picturesque retreat.

Alhamis ya kutupia za nyuma..

nikiangalia hii picha ya mtu wangu mdogo alivyokuwa ana graduate huwa nafurahi na kujipongeza. kwanza, najipongeza kwa kuwa kumhangaikia mtu mpaka a graduate si mchezo. pili, nafurahi na kujichekea mwenyewe kwani anavyopokea hicho cheti kwa kuonyesha "white dent" utadhania anaelewa kwa sana kinachoendelea.

Wednesday, October 16, 2013

My article for newspaper: Zingatia haya kabla ya kununua shuka



Shuka ni kitu rahisi tu ila kama unasoma makala hii, ni kuwa unajisikia kuzidiwa nguvu na aina zilizopo au umechoka kufanya manunuzi mabaya. Usingizi mzuri wa usiku una matokeo makubwa ya ni jinsi gani unafanya kazi na kujisikia wakati wa mchana, na shuka unazolalia zinachukua nafasi kubwa ya kilele cha matokeo haya. Zaidi pia ni kuwa unataka kununua shuka ambazo zinatosha godoro na zisizochakaa mapema.

Ni kitu gani cha kwanza ambacho mtu anaona wakati anapoingia kwenye chumba chako cha kulala? Bila shaka ni kitanda. Ni ajabu kama utakuwa na chumba cha kulala kisichokuwa na kitanda. Pengine kitanda ndio sababu kubwa inayofanya uite chumba hiki kuwa ni cha kulala! Unaweza ukaboresha muonekano wa chumba chako cha kulala kwa kutandika kitanda shuka laini na kufunika kwa duveti tu bila kugusa maeneo mengine ya chumba. Hii inakupa maboresho ya chap chap kwa hivyo kuokoa muda na pesa.

Kuna rangi na mitindo mingi ya shuka sokoni. Unakumbuka wakati shuka zote zilikuwa ni za pamba na ni za kijani? Kama ndio basi bila shaka utakuwa unapigwa na butwaa ni shuka za aina ngapi zilizopo sokoni leo hii. Unaweza ukaongeza rangi, staili na michoro mbalimbali kwenye chumba chako cha kulala kwa kutumia shuka na duveti za kisasa. Endelea kusoma hapa ili ujue ni nini cha kufanya kabla hujatumia hela yako ya thamani kununua shuka mpya.

Pima ukubwa wa kitanda chako. Kuna uwezekano mkubwa umeshasikia hiyo lugha ya vitanda vya ukubwa wa twin, au queen au king. Usidanganyike na majina haya ya vitanda, kiukweli ni kuwa hakuna vipimo sahihi vya kitanda kwa majina haya. Sasa kabla hujaenda kununua shuka, pima kitanda chako kwa umakini ukichukua vipimo kutoka kichwani hadi miguuni, upande kwa upande na unene wa godoro. Kuwa na uhakika unajua kwa usahihi ni nini unahitaji kabla ya kununua.

Shuka nyingi zinauzwa kwa hayo majina kama hayo yanayoweza kukuvutia hapo juu kuhusu ukubwa wa kitanda. Usidanganyike, kwa kuwa tayari una vipimo sahihi vya kitanda chako, kama ni ile aina ya shuka ya kufitisha kuvalisha godoro hakikisha inazidi inchi mbili ya vipimo ulivyo navyo ili kuwa na kitambaa cha kutosha kusaidia kuvalisha kona za godoro. Kama ni aina ile ya shuka ambayo ni flati basi hakikisha kinaongezeka kitambaa cha kutosha cha kuchomekea ili shuka isikimbie godoro unapokuwa umelala. Kuwa makini, wataalamu wanasema shuka nyingi zinapungua kwa asilimia saba ya ukubwa wake baada ya kufuliwa kwa mara ya kwanza, na shuka zenye asilimia mia ya pamba zinapungua zaidi!

Shuka nyingi zinawekwa rangi baada ya nyuzi zake kusukwa, ambapo inazifanya kuwa ngumu mpaka baada ya kufuliwa mara kadhaa. Zile shuka zinazotengenezwa na nyuzi zilizotiwa rangi kabla ya kusukwa huwa ni laini na ni za bei kubwa zaidi.
Soma maelezo ya lebo ya mtengenezaji wa shuka husika, yatasema wingi wa nyuzi zilizotumika kutengenezea kwa kila inchi moja ya mraba. Baadhi ya wanunuzi hawajui kuhusu wingi wa nyuzi na pengine shuka zinapitishwa na muuzaji (labda ni ofsini muda wa chakula la mchana) watu wananunua bila kusoma maelezo. Wingi wa nyuzi unasababisha ubora wa shuka. Kwa kiwango cha kitaalam wingi wa nyuzi uwe zaidi ya 250 na usiwe chini ya 175. Kwa shuka ambazo utalalia kila, raha jipe mwenyewe, nunua zenye ubora wa juu kwa kiasi ambacho utamudu. Zaidi ya yote ni imani kuwa utatumia saa nane kwa siku ukiwa umezilalia!
Ukiwa unanunua shuka mguso wa kitambaa ni muhimu pia. Pamba ni kitambaa cha shuka ambacho ni maarufu zaidi, ingawa baadhi ya watu wanapendelea shuka zenye mchanganyiko wa pamba na labda satini ama hariri ama polista ili kupunguza kujikunja kunja. Shuka za mchanganyiko wa pamba na polista ni imara zaidi na hazijikunji kunji ila changamoto yake  ni kupoteza ulaini na ni ngumu kuondoa madoa ukilinganisha na pamba tupu.
Angalia maelezo ya ufuaji. Labda shuka unazotaka kununua ni ambazo ni lazima zifuliwe kwa mafuta maalum tu (hazifuliwi na maji) hivyo kutakuwa na gharama ya kuzipeleka dry cleaner kila wiki. Je utamudu hiyo? Hakikisha utaweza kutunza shuka zako jinsi mtengenezaji alivyopendekeza. Zitadumu muda mrefu na hata kama ikitokea tatizo na ukiwarudishia wakijiridhisha kwamba zilikuwa zinatunzwa inavyotakiwa watakusikiliza.

Amua kama unataka kununua shuka zako kwa seti ama moja moja. Nunua nyingi kuliko unazohitaji. Kama umetumia muda mwingi kutafiti na kupata jibu la ni shuka zipi unahitaji huna haja ya kufanya zoezi hilo tena ndani ya kipindi kifupi. Fikiria kununua seti mbili ama tatu ambazo zinaendana kwa ajili ya kubadilisha ili hata kama mtu amemwaga kitu kwenye shuka la juu unalibadili hilo peke yake bila kuhusisha la chini.

Pata muonekano na weka staha kwenye chumba chako cha kulala kwa mvuto wa juu kwa rangi na mitindo mbali mbali ya shuka, mwisho wa siku ni wewe unalala humo. Na kinachojalisha zaidi wakati huo ni burudani. Hutaweza kulala kwa raha kama huna matandiko  laini na safi.

Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi anajishughulisha na usafi wa mazulia, nguo na magari; pia ana mapenzi makubwa ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk

Tuesday, October 15, 2013

anayem bana anamwezea!

hii nayo utaipenda..ni katika maandalizi ya sikukuu kesho. bishost amenitonya kuwa hata kama wewe unataka kubanwa hivi nistue nimwambie. watu kweli hodari kwa kazi zao!!





Monday, October 14, 2013

Hizi ni baadhi ya nyumba Mwl alizowahi kuishi

tukiwa tunasheherekea maisha ya Baba wa Taifa la Tanzania leo haya ni baadhi ya yaliyokuwa makazi yake
aliishi kwenye nyumba hii kwa siku 14 tu akaondoka kwenda kwenye matibabu Uingereza ambako alifariki October 14, 1999
 hii ndiyo nyumba ya Mwalimu Nyerere aliyokuwa akifikia alipokuwa akisafiri kwenda Butiama akiwa kama Rais wa Tanzania kati ya miaka ya sitini hadi miaka ya themanini mwanzoni

hii ni nyumba ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) ilimjengea Mwalimu katika miaka ya themanini. Nyumba hii ilijengwa kwenye eneo la mwinuko la Mwitongo kijijini Butiama. ni nyumba ambayo Mwalimu Nyerere aliishi kwa kipindi kirefu baada ya kustaafu uongozi wa Serikali akiwa kijijini Butiama


nyumba iliyojengwa kuzungukia kaburi la Mwalimu Nyerere, eneo la Mwitongo, Butiama
picha kwa hisani ya wavuti