Pages

Tuesday, March 18, 2014

news: ukwepaji gharama huchangia kuwepo majengo yasiyo na ubora

UKWEPAJI wa gharama za ujenzi wa nyumba, unadaiwa kuchangia kuwepo majengo yasiyo na ubora katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 
Katika ukwepaji wa gharama, wengi hukwepa kutumia wataalamu wa majengo, hususan wabunifu wa majengo na wakadiriaji majenzi waliothibitishwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi nchini, Jehad Abdallah Jehad alisema hayo leo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habar.
Alikuwa akizungumzia semina endelevu ya Bodi itakayofanyika jijini Mbeya Machi 20 na 21. Alisema ni nyumba chache zilizojengwa kwa ubora. Jehad alisema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa ujenzi wa nyumba ni gharama kubwa tofauti na wengi wanavyodhani.
“Ujenzi wa nyumba ni sawa na mgonjwa anayehitaji tiba hospitali. Usipomuona daktari kwa ajili ya vipimo badala yake ukaenda duka ladawa watakuandikia dawa tu lakini ugonjwa bado utakuwa palepale,” alisema.
Alisisitiza, “wananchi wasiogope gharama za kutafuta wataalamu. Hawa ni watu waliosomea kwa muda mrefu taaluma hiyo, hivyo tunawaasa wawatumie wataalamu hawa ili kupata majenzi yenye ubora.”
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk Ambwene Mwakyusa alisema wameandaa utaratibu wa semina endelevu kwa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi katika miji mbalimbali nchini .

No comments:

Post a Comment