Pages

Friday, February 20, 2015

Chupi inayobana yamtoa mbunge bungeni


Mbunge mmoja wa Canada alitoa sababu ambayo haijawahi kusikika iliomlazimu kutoka bungeni kwa haraka.

Amesema kuwa suruali yake ya ndani ndio iliomlazimu kuondoka mapema kwa kuwa ilikuwa ikimbana.
Mbunge huyo wa upinzani Pat Martin alimwambia Spika kwamba vazi hilo lilimbana sana na kumzuia kuweza kuendelea na kikao cha kupiga kura.

Hata hivyo alifanikiwa kurudi kwa wakati na kupiga kura yake.

Baadaye mtandao wa twitter ulijaa ujumbe wa kisa hicho.
Mbunge huyo alizua ucheshi miongoni mwa wabunge wenzake liposema kwamba alinunua suruali hiyo kwa bei ya chini bila kujua kwamba ilikuwa ndogo.

Spika wa bunge hilo alisema kwamba alimuagiza mbunge huyo kuketi chini wakati alipotaka kutoka.
Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment