Pages

Thursday, February 5, 2015

Inasikitisha sana, askari Polisi PC Joseph Swai, ameuawa wakati akimwokoa mtoto wa miezi minane

Mara nyingi visa kama hivi visababishwa na mwanaume kuamini kuwa mtoto si wake, lakini kwanini usiende kwenye vipimo au kuwafukuza tu mtoto na mama yake kuliko kuua mtoto wa miezi nane jamani?

Nipashe linaripoti kuwa:
Askari Polisi PC Joseph Swai, ameuawa wakati akimwokoa mtoto wa miezi minane, aliyekuwa akiteswa na baba yake mzazi katika mtaa wa Chang'ombe Juu mjini hapa.
 
Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 5:00 asubuhi na kumtaja mtoto aliyekuwa anateswa kuwa ni Valerian Mallya.
 
Alisema awali, polisi huyo alipigiwa simu na Mtendaji wa mtaa wa Chang'ombe Juu, akimjulisha kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Oliva Baltazar (52), kuwa kijana wake, Tisi Mallya (29), anamtesa mtoto wake.
 
Alisema polisi huyo alikwenda eneo la tukio na alipofika aligonga mlango huku akijitambulisha kuwa ni askari, kisha akamuamuru atoke nje.
 
Hata hivyo, alisema Mallya alimnyanyua mtoto wake huyo kwa mkono mmoja miguu ikiwa juu na kichwa chini, akitishia kumuua kwa panga.
 
Kamanda Misime alisema askari huyo aliamua kumwokoa mtoto huyo kwa kumrukia mtuhumiwa lakini aliteleza na kuanguka chini na ndipo mtuhumiwa huyo alipopata mwanya wa kumkata kichwani na maeneo mengine ya mwili.
 
Alifafanua kuwa mama na mwanawe walifanikiwa kutoroka bila kupata madhara yoyote.
 

Kamanda Misime alisema baada ya mtuhumiwa kufanya unyama huo, alikimbia akiwa ameshika panga lililokuwa limetapakaa damu na polisi wanaendelea kumtafuta ili afikishwe mbele ya vyombo vya sheria kujibu mashitaka yanayomkabili.

No comments:

Post a Comment