Pages

Friday, February 13, 2015

MAHUSIANO: Enyi wake watiini waume zenu, kwa kila kitu?


Nachukulia mfano wa picha hizi japo tamaduni zinatofautiana lakini naongelea hapa katika angle nyingine. Kim anapendezaga sana lakini hapa hajapendeza hata,
alivyovaa head to toe ni mavazi ya mume wake anayoonyesha kwenye shoo New York (hivi zipo marks za kuwa fashion designer?)Labda, narudia tena labda kwa mawazo yangu ameona kabisa hapana lakini amevaa hivyo kumtii mumewe. Sasa najiuliza hivi mke kuambiwa amtii mume wake ni kwa kila kitu hata kile kinachoonekana hapana, wanasema akili za kuambiwa changanya na za kwako. Sasa ikiwa ni ndio ndio tu si kutakuwa hakuna changamoto na maisha yataboa? Yani kila kitu ndio tu kama ndondocha? 

Mavazi hayo ya Yeezy, kazi kwako fashionista
nasikia alivyoona aibu wala hakuvua hilo koti

huyoo anaondoka,nadhani hapo kina kwin B wanashanga ni nini hiki leo,..

No comments:

Post a Comment