Pages

Friday, February 13, 2015

Maskini! Huyu kaka amefiwa na mama, baba na watoto wawili kwenye ajali ya mtoto kipunguni

Hawa ni watu wa karibu mno mtu kuondokewa kwa siku moja, Mungu amtie nguvu.
Ndugu wa Emmanuel Mpira (katikati) wakimfariji katika nyumba ya jirani jana, baada ya kupoteza ndugu zake sita walioteketea kwa moto usiku wa kuamkia juzi Jumamosi, Kipunguni Dar es Salaam. 

Mpilla alipoteza ndugu hao sita, akiwamo mama na baba yake, kaka yake, watoto wake wawili na mjomba wake katika tukio ya nyumba kuungua moto lililotokea usiku wa kuamkia Februari 7, Kipunguni A, Dar es Salaam.
Familia ya kijana Emmanuel Mpilla (27),  aliyepoteza ndugu sita katika ajali ya moto, imepanga kumpa tiba ya kisaikolojia ili kuirudisha akili yake katika hali ya kawaida.

Mpilla alipoteza ndugu hao sita, akiwamo mama na baba yake, kaka yake, watoto wake wawili na mjomba wake katika tukio ya nyumba kuungua moto lililotokea usiku wa kuamkia Februari 7, Kipunguni A, Dar es Salaam.

Tangu kutokea kwa msiba huo, Mpilla hakutaka kuzungumza lolote, hali inayoonyesha ameathirika kisaikolojia.
Akizungumza kwa niaba ya familia, baba mkubwa wa Emmanuel, Merikioli Mpilla alisema uamuzi wa kumpa tiba ya kisaikolojia kijana huyo ulifikiwa katika kikao cha wanandugu kilichofanyika jana.

“Kuna mambo mengi ya kifamilia, tulipaswa tuyajadili, lakini kwa kifupi yanayomuhusu Emmanuel ndiyo yalitawala kikao,” alisema Mpilla. CHANZO Mwananchi

No comments:

Post a Comment