Wabunge wa bunge la Uingereza wameunga mkono
sheria inayoruhusu uzaaji wa wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka kwa wanawake
wawili na mwaume mmoja, katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria zinazoruhusu watoto
wenye vinasaba vya watu watatu tofauti.
Wakati wa mjadala huo, mawaziri wamesema mbinu hii ni "mwanga kwa
safari ndefu ya giza" kwa familia kupata watoto.
Upigaji kura zaidi unahitajika katika baraza la bunge la juu, maarufu kama
House of Lords. Iwapo kila kitu kitakwenda sawa, basi mtoto wa kwanza wa
teknolojia hii atazaliwa mwaka ujao.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron anasema: "Hatuzungumzii Mungu
hapa, tunahakikika kuwa wazazi wawili ambao wanataka mtoto mwenye afya wanaweza
kumpata."
No comments:
Post a Comment