Pages

Friday, March 20, 2015

AJALI YA BASI YAUA 7....IMETOKEA ENEO LA MIKUMI KATI YA BASI LA MSANGA LILILOKUWA LINATOKA DAR KWENDA MAHENGE NA LA LUWINZO LILILOKUWA LINATOKA NJOMBE KWENDA DAR

Watu saba  wamefariki dunia  na wengine  zaidi  ya 48 kujeruhiwa vibaya  baada  ya  basi  la Msanga Line walilokuwa  wakisafiria  kugongana uso kwa uso na basi  la Luwinzo  katika eneo la  hifadhi ya  taifa  ya Mikumi, wilaya  Kilosa, Morogoro.

Ajali  hiyo  ilitokea jana saa 6:45 mchana, baada ya basi la Msanga  Line  linalosafiri Dar es Salaam kwenda Mahenge, wilayani Ulanga, Morogoro kugongana na basi la Luwinzo lililokuwa linatoka Njombe  kwenda Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Poul (pichani), chanzo cha  ajali  hiyo  ni mwendo  kasi wa madereva wa mabasi  yote ambayo walishindwa kuyamudu.
Alisema majeruhi wengi wa ajali  hiyo wamelazwa katika hospitali ya  Mtakatifu Kizito wakisubiri  utaratibu wa  kupelekwa katika Mospitali  ya  mkoa wa Morogoro.
Alisema miili ya marehemu haijatambuliwa na imehifadhiwa katika  chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo. Chanzo: Nipashe

No comments:

Post a Comment