Pages

Tuesday, March 10, 2015

INASEMEKANA HAYA NI MAENEO YA BAFUNI AMBAO WENGI WANASAHAU KUYASAFISHA...JE NAWE PIA WASAHAU MOJAWAPO?

1. Shower curtain - hii kwakweli hadi ishushwe kusafishwa inaweza kaa hata mwezi kwa baadhi ya watu. Hasa kama ina rangi ya brown na ile michoro la makonokono ya baharini basi hadi ianze
kuteleza kwa utando maeneo ya chini ndio mtu anashtuka loo...hii kitu ifunguliwe ikafuliwe sasa. Pazia la bafuni linafaa lifuliwe kila wiki.

2. Kile ki trash can cha bafuni - hiki huwa kinamwagwa na kubadilishwa mfuko lakini wengi wanasahau kukisafisha chenyewe kama chenyewe.

3. Chini ya sink - kuna yale masinki yenye nguzo iliyoshikilia ambapo iko wazi kwa nyuma kutazamana na ukuta. Ukiinama ukagusa pale unakuta mabuibui ya kufa mtu na hata yale mabaki ya zege na vumbi la cement la wakati wa ujenzi wa  hilo bafu miaka kadhaa iliyopita bado lipo. Yani hakujawahi kufikwa maji toka bafu lianze kutumika.


4. Holder ya brash ya kwenye bakuli la choo - wengi huwa wanasafisha kwa juu wakati wakiweka brashi, lakini kwa chini kuko wazi na wengi huwa hawakigeuzi kusafisha.

5. Pale pa kutundikia toilet paper - Ni eneo dogo ambalo halipati uchafu mwingi lakini panakuwa na vumbi. Unaposafisha bafuni kumbuka kupafuta.

No comments:

Post a Comment