Pages

Monday, March 2, 2015

KUTOKA KWANGU: Hatua 5 za kusafisha bafu lako ling'ae

Bafu linaweza kuwa ndicho chumba kigumu zaidi kusafisha. Kufanya kazi moja kwa hatua itakusaidia kumaliza bafu zima fasta. Hizi ni hatua tano za kufanya kila mahali pawe safi bafuni.

Hatua ya 1:  Weka dawa za kusafishia zile sehemu sugu, kwa mfano nyunyiza vim kwenye taili zenye ukurutu
Hatua ya 2: Safisha sinki na kioo
Hatua ya 3: Safisha  choo
Hatua ya 4: Safisha shower na tub
Hatua ya 5: Safisha sakafu na mwaga taka

Vifaa unavyohitaji
Dekio/mopper + ndoo
Sponji
Brushi ya kusugulia kwenye taili
Brashi ya kusugulia kwenye bakuli la choo
Kitaulo kikavu cha kufutia
Sabuni na dawa za kusafishia bafuni
Dawa ya kusafishia kioo
Na of course maji.

Kuna ambacho nimesahau labda?


Hongera! Umeweza kumaliza kusafisha bafuni fasta, nenda kanywe juisi ama lala kidogo! Unastahili!


No comments:

Post a Comment