Pages

Thursday, March 12, 2015

MAHAKAMA YAKUBALI KUONDOLEWA KWA ASKOFU NA WACHUNGAJI WAWILI KWA KUKIUKA KATIBA YA KANISA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali kuvuliwa nyadhifa kwa Askofu wa Kanisa la Elim Pentekoste, Dayosisi ya Pwani, Manaseh Martin na wachungaji wawili, Tito Tunda na Jarome Andrea, kwa sababu ya
kukiuka katiba ya kanisa hilo na kwenda kinyume na mahubiri.

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Binge Mashabara baada ya kukubali hoja za Baraza la Wadhamini la kanisa hilo ambalo lilikuwa limefungua shauri hilo dhidi ya askofu na wachungaji hao.

Akitoa uamuzi huo alisema walalamikiwa hao wanaondolewa kwenye nafasi zao za uaskofu na uchungaji, pia wanatakiwa kurudisha mali zote ikiwemo vitabuvya benki, magari waliyokuwa wanashikiri aidha walalamikiwa wanatakiwa kulipa Sh milioni 10 kama gharama ya usumbufu na madhara ya jumla.

Hakimu Mashabara alisema nI aibu kwa viongozi wa dini kugombea madaraka kama wanasiasa au wananchi wa kawaida ambao wanawategemea kama viongozi wa kiroho pia wameaminiwa na wananchi kuwaongoza dhidi ya uovu na vurugu katika jamii hivyo walitakiwa wawe mfano bora na kuibadilisha jamii ili iwe na mwelekeo mwema.

Alisema mahakama imekubali kuwa uamuzi uliofanywa na walalamikaji kuwaondoa madarakani walalamikiwa ulikuwa sahihi kwa mujibu wa katiba dhidi ya vitendo vyao ambavyo vinapingana na mafundisho ya dini yao. 
  
Kwa mujibu wa hati ya madai iliyofunguliwa mahakamani hapo na mawakili kutoka Kings Law Chambers Novemba 25, 2011, na Baraza la Wadhamini la kanisa lilimwondoa madarakani Askofu Manaseh kwa sababu ya kwenda kinyume namaadili, katiba na mafundisho ya dini hiyo.

No comments:

Post a Comment