Pages

Tuesday, March 17, 2015

MAMBO YA NGONO BWANA....HAYANA CHEO WALA TAALUMA....MAJAJI WATATU NCHINI UINGEREZA WAFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA KUTUMIA MUDA WA OFISI KUTIZAMA FILAMU ZA NGONO

Jaji Timothy Bowles anayesikiza kesi za wilaya , jaji wa maswala ya uhamiaji Warren Grant na jaji Peter Bullock wamefutwa kazi.

Majaji hao walipatikana na hatia ya kutumia mtandao rasmi wa mahakama kwa
mujibu wa wachunguzi wa idara ya mahakama.

Maafisa hao wanasemekana kuwa walitazama mitandao yenye filamu za ngono huku wakifahamu vyema kuwa ilikuwa ni ukiukaji wa sheria za matumizi kwa mujibu wa msimamizi wa idara hiyo ya Mahakama.

Hata hivyo kiongozi wa idara ya mahakama hiyo ya Uingereza na jaji mkuu waliwapata na hatia ya kwenda kinyume cha maadili ya mahakama.

Jaji wa nne Andrew Maw aliamua kustaafu mwenyewe wakati uchunguzi huo ukiendelea badala ya kufikishwa kizimbani.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisheria Clive Coleman alisema kuwa makosa hayo yalikuwa makubwa sana katika mizani ya uadilifu wa majaji.

Aidha hakuna hata mmoja wao atakayeruhusiwa kufanya kazi katika idara ya mahakama tena.



No comments:

Post a Comment