Pages

Friday, March 20, 2015

MSIOOA PITENI HAPA KUNA UJUMBE WENU MZITO

Kama wenyewe wanavyojiita kichwa cha nyumba mwanaume kabla ya kuoa kuna mambo muhimu ya kujipima kabla ya kukurupuka kusema anaoa.

Wanawake siku hizi siyo kama wa zamani
ambapo wanachojali ni kuolewa na mwanaume mwenye manguvu anayeweza kulima na kupata mazao ya chakula cha familia, siku hizi usalama wa familia una mambo mengi na mambo hayo yanahitaji fedha. 

Sasa kama mwanaume anataka kuoa ni lazima ajipime kwa haya mambo yafuatayo;

1. Awe na uhakika wa kipato cha kutosha kutunza familia iwe ni kazi nzuri au biashara iliyosimama vyema itakayomhakikishia kwamba atamudu kuhudumia familia yake.


2. Ajifunze kudhibiti hasira zake kwani kuishi na mwanamke kunahitaji busara na siyo kulipukwa na hasira kusiko na sababu.

3. Kama alikuwa ni mtu wa totoz basi aseme imetosha abadilike na kuzaliwa upya ndoa na uzinzi haiwezi kuwa na amani na hata baraka katika familia haitakuwepo mwanaume anaweza kujikuta kila siku ana mgogoro wa kifedha hata kama kipato chake ni cha kuridhisha.

4. Ajifunze kuishi kama mtu mzima, aachane na vijiwe na makundi ya wahuni wanaokesha kwenye vilabu vya usiku, abadilishe marafiki na kujenga urafiki na watu wazima waliomtangulia katika ndoa miaka kumi au hata ishirini watamsaidia kukua kifikra.

5. Kujenga uaminifu kwake na kwa mwenzi wake kwani kama wote mmeamua kuishi pamoja ni lazima mliaminiana hivyo kuanza kujenga kutoaminiana inaonyesha mlikurupuka, na hiyo ndoa kamwe haitakuwa na amani. Ni vyema kabla ya kuingia kwenye ndoa muwe na uhakika kama kila mmoja anamuamini mwenzake, na kamwe usije ukaoa mtu usiyemuamini ni kutaka kuishi kwa jakamoyo.

6. Mwanaume anatakiwa ahakikishe anakuwa na chaguo zuri, mapenzi ya kuhemkwa hasa baada ya kukutana kimwili wakati mwingine hayatupi uchaguzi mzuri, ni vyema msomane na kuwa na uhakika kama huyo unayetaka kumuoa anafikia matarajio yako.

Kumbuka huoi malaika lakini angalau sifa njema zivuke asilimia 50 na hizo nyingine mtamudu kukamilishana, usijidanganye kwamba utapata mwanamke mkamilifu kwa asilimia zote, lazima kutakuwa na maeneo hutaridhishwa nayo kwa hiyousije ukajidanganya kwamba utamudu kumbadilisha.

Si kweli kama ni kubadilika aamue mwenyewe na kama hatabadilika basi ukubali kwa sababu hata mwenzi wako naye kuna maeneo pia atakuwa haridhishwi nayo kwa hiyo hapo ni win win situation.Lakini pia usije ukachagua mwenza kwa sifa za nje.

Kumbuka sifa za nje zinaweza kutoweka upendo wote ukaisha kwa sababu ulichokuwa ukikipenda hakipo, unatakiwa uanze na sifa za ndani za nje iwe ni nakshi tu kwamba inaweza iwepo au isiwepo na upendo ukaendelea kama vile manukato, yawepo yasiwepo mwanamke ni yule yule.


7. Kuwa mtu mwema ni muhimu kuwathamini watu kwa utu wao siyo kwa kile walicho nacho,ukianza kuwathamini watu kwa kile walicho nacho au wanachomiliki jambo hilo litakuletea matatizo mbele ya safari. Daima kuwa wewe halisi usiigize, usiwe na kiburi au mtu wa kujivuna au kujidai na kupenda sifa, hutakuwa na mahusiano mazuri na mwenzi wako na pia watu waliokuzunguka

8. Je unajua kupika? Kama mwanaume hajui kupika kwa sababu alizoea kula kwenye vibandavya chipsi au magengeni au kwenye Baa, basi ni vyema akaanza kujifunza kupika. Kuoa hakumaanishi kwamba unaoa mpishi maana kuna neno moja mnapenda kulitumia pale mnapooa mnapodai mmepata jiko.

Zamani mwanamke alichukuliwa kama mtu wa jikoni lakini siku hizi mwanamke siyo lake jiko bali ni jiko lenu kwa hiyo ili kunogesha mapenzi yenu ni vyema mara moja moja mwanaume amshangaze mwenzi wake kwa mapishi. Lakini pia pale mwenzi wake atakapoumwa mwanaume awe na uwezo wa kuingia jikoni na kupik
a

9. Kutokuwa msiri kwa mwenzi wako, Kama ulikuwa na mipango yako au kuna miradi yako unayoifanya, pale utakapochagua mwenza ni vyema ukaanza kumshirikisha kwa kila hatua unayopiga, kumbuka huyu ni mtu uliyemuamini, hivyo ni vyema ukawa unamshirikisha kwa kila hatua unayopiga ili kesho na kesho kutwa umepata dharura mambo yako hayatasimama.

10. Je una ukaribu gani na Mungu? Wakati mwingine kutokana na sarakasi za ujana mwanaume anaweza kujikuta akiwa amemsahau Mungu, ni vyema kabla ya mwanaume kusema anaoa ahakikishe anamrudia Mungu kwa kuzaliwa upya na kuwa muumini mzuri wa dini yake. Kwa kuwa karibu na Mungu maisha yake na mwenzi wake yatakuwa yafuraha na amani na hata watoto watakaozaliwa na kukuzwa kiroho watakuwa namaadili na manufaa kwa jamii iliyowazunguka.

Hii iwafikie wanaume wasiooa.

CHANZO JAMIIFORUM

No comments:

Post a Comment