Pages

Friday, March 20, 2015

NIKO TAYARI KUWA BABA WA KAMBO WA WATOTO WA SALIMA:...LINEX

Nimesoma hii habari nikabaki na maswali kichwani....Tuseme wewe ni mama na una watoto, halafu aliyekupenda zamani ambaye sio baba wa hao watoto akasema anatamani siku moja aje kuwa baba wa kambo wa watoto wako kwa ajili alikupenda sana mwanzo. Je tafsiri yake ni kuwa anatamani baba wa watoto wako wa sasa afe ama muachane ama tafsiri yake sahihi ni ipi labda?

Msanii wa muziki wa bongo fleva Sunday Mjeda maarufu kama Linex ambaye anatamba kwa sasa na wimbo wake mpya wa Salima leo amefunguka kupitia kipindi cha Clouds360 na kusema idea ya wimbo huo imetokana na Salima
ambaye alikuwa rafiki yake wakati anasoma Shule ya msingi na alikuwa msaada wake katika baadhi ya vitu vya shuleLinex aliendelea kufunguka na kusema Anatamani siku moja aje kuwa Baba wa kambo wa watoto wa Salima kwani anaona anampenda Salima kiukweli japo Salima hataki ata kuongea naye alisema Linex kwenye mahojiano na Clouds360

No comments:

Post a Comment