Pages

Friday, March 13, 2015

MUME ACHOMWA MOTO KWA Kumkumbuka marehemu mkewe....ASEMA WANAUME MNAPOTESWA AU KUPIGWA NA WAKE ZENU HAMPASWI KUONA HAYA....


Yaleyale...wapendanao wakigombana pita mbali..mapenzi dunia mzima kama vile yanafanana..
Mwanaume aliyechomwa na maji moto kwa kumkumbuka marehemu mke wake wake amesema kuwa haoni haya kamwe kwa kitendo alichofanyiwa na mpenzi wake.

Ken Gregory, 65, anayetokea Peterborough, Uingereza amesema kuwa wanaume wanaopondwa kuteswa ama hata kupigwa na wake wao hawapaswi kuona haya.

Yamkini Gregory alikuwa amepanga kutembelea kaburi la mke wake kwa sababu ilikuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake lakini hoja hiyo ikapingwa
na mke wake wakati huo Teresa Gilbertson, 60 .


Wawili hao waliteta na kupelekea Teresa kumwagia maji yaliyochemka.
Wawili hao Gregory na bi Gilbertson walikutana miaka 7 iliyopita baada ya kifo cha mpenzi mke wake wa mika 30, Maureen.

Lakini kilichozua ubishi na hatimaye janga ilikuwa ni wazo tu ambayo bi Teresia anasema aliona kama hapendwi tena na akaamua bora waachane iwapo
Bwana Gregory ataendelea kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mpenziwake wa zamani japo ni Marehemu.

Gilbertson aliondoka kwenda kupika chai lakini akarejea akiwa amefoka na buli la maji moto ambayo alimwagia mumewe kutoka nyuma.

Bi Teresa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha maumivu na uchungu mwingi kwa mumewe ambaye amemtaliki.


Gilbertson atahukumiwa tarehe 24 Mach. Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment