Pages

Friday, March 13, 2015

NUHU MZIWANDA: SHILOLE anipige tu.....HAKUNA SHIDA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nuh Mziwanda, ametoa kali ya mwaka kwa kudai kwamba kitendo cha kupigwa mara kwa mara na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kinampa furaha
na ufahamu wa namna anavyopendwa.

“Kwanza kupigwa raha, mpenzi wako asipokupiga hakuonei wivu, mimi nafurahi sana na namtaka anipige tu! kila siku akijisikia, ananidhihirishia kuwa ananipenda,” alisema.

Nuh alisema mengi yamesemwa kutokana na kupigwa kwake mara kwa mara, huku akidai kwamba hilo halina tatizo kwake, kwa kuwa halitaharibu mapenzi yao wanayoamini yatafika mbali.


“Sisi tunawezana na Mungu atusaidie tufikie katika hatua ya ndoa tuliyojiwekea,’’ alimaliza. KUTOKA MTANZANIA

No comments:

Post a Comment