Pages

Wednesday, March 4, 2015

Nay wa Mitego aweka wazi majibu ya "ngoma", asema alishawahi kuchepuka huku akiwa na Siwema

Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego hivi karibuni aliweka wazi majibu yake baada ya kupima UKIMWI kupitia account yake ya Instagram na kwamba alikuwa yupo safi yaani(Negative).
Alipoulizwa sababu ya kupima ngoma alisema kuwa alikuwa akiumwa ugonjwa wa Malaria na alikuwa hajaugua kwa muda mrefu na alipokwenda hospitali ilibidi apime na ngoma ingawa ni kawaida yake kupima mara kwa mara.

‘’Nilipima baada ya kuumwa Malaria lakini huwa ni kawaida ya kupima ngoma hata mke wangu(Siwema) alipokuwa mjamzito tulikwenda pamoja kupima hospitali,’alisema Nay. Alipoulizwa kama tangu alipoanza uhusiano na mke wake Siwema alishawahi kuchepuka alisema kuwa ni kweli alishawahi kufanya hivyo ila hawezi kusema ni mara ngapi ili kunusuru ‘ndoa’ yake.


‘Unajua ni mambo ya ujana ni kweli nilishawahi kuchepuka lakini siwezi kusema ni mara ngapi si unajua mama watoto anaweza kukasirika? Lakini nilikuwa makini sana na namwomba sana msamaha mke wangu na sitegemei kuchepuka tena,’’alisema Nay.

No comments:

Post a Comment