Pages

Wednesday, March 18, 2015

WENGI WANA MAONO NA WANAJUA NI NINI WANACHOTAKA KUPAMBA KWENYE NYUMBA ZAO....TATIZO NI BAJETI...PATA DONDOO YA JINSI YA KUVUKA KIZINGITI HIKI

Ingawa wengi wetu wana ladha na matamanio yao binafsi ya vile wangependa maeneo mbalimbali ya nyumba zao yaonekane, tatizo linaweza kuwa bajeti. Yani unaenda kwenye show room ya home decor unatamani kweli lakini pesa haitoshi. Nimejifunza dondoo moja itakayokuwezesha kupamba bila bajeti kubwa. Mbinu hii hapa:

Weka hela nyingi kwenye ile fenicha ambayo ni ya kudumu ambayo ni sofa. Hukuti mwenye nyumba akibadilisha sofa kila baada ya miaka miwili au mitatu labda awe ni mtu wa kuhamahama. Hata kama ni kuwa watoto wamekuwa kwahivyo hawaharibu tena vitu, sanasana ni kuwa atabadilisha sofa kati ya miaka kumi na hata kumi na tano na wengine sofa ni za lifetime. Kwahivyo unajikuta kuwa hakuna ubaya kuweka hela ya maana kwa fenicha ambayo utadumu nayo zaidi ya miaka 10

Ukishawekeza hela yako hiyo ya maana kwenye sofa ,then vile vitu vingine vidogo dogo vya mapambo kama vile taa, vioo na vitu vya kwenye display cabinet huna haja ya kununua vya bei ghali. 

Ukivipangilia kwa pamoja sebule yako itaonekana mwaaa kwa kunyanyuliwa tu na sofa zenye kiwango.

No comments:

Post a Comment